Na Friday Simbaya, Iringa IMEELEZWA kuwa uelewa mdogo wa matumizi sahihi ya chakula pamoja na kutokula chakula mchanganyiko na kutumia nafaka kutengenezea pombe za kienyeji, ndio sababu za kuwepo kwa tatizo la utapiamlo katika Mkoa wa Iringa. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakati wa kufungua mkutano wa kamati za lishe za halmashauri na mkoa kuhusu masuala ya lishe ya mama na mtoto jana. Mkutano huo wa uhamasishaji masuala ya lishe kwa watendaji ngazi ya mkoa na halmashauri uliaandaliwa na Mradi wa Lishe wa Mwanzo Bora (Mwanzo Bora Nutrition Program) kwa ufadhili wa serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la maendeleo ya kimataifa (USAID). Mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa matatizo mbalimbali ya utapiamlo yanaendelea kudumaza, kulemaza na hata kuua watoto na wanawake hasa wajawazito na wanaoyonyesha. Pia jamii kwa ujumla imekuwa ikiathirika kwa njia moja au nyingine kwa kuwepo kwa utapiamlo. Alisema kuwa tataizo la lishe duni ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.