Skip to main content

Posts

Showing posts from March 1, 2026

QUALIFYING TEST ( For Private Candidates Only )

PROF. JANABI AZINDUA WODI YA WATOTO NJITI HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA, MWANZA

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Prof. Mohamed Janabi amezindua wodi ya kwanza na ya kisasa nchini kwa ajili ya watoto njiti, iliyojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Prof. Janabi amefanya uzinduzi huo jumamosi Februari 28, 2028 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO,  Dkt. Tedros Ghebreyesus ambapo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 2.125 ikijumuisha jengo, vifaa tiba na mbili nyumba za watumishi. Prof. Janabi ametumia fursa hiyo kuipongeza  taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation- DMF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Keep a Child Alive (KCA) na  Shirika la JHPIEGO   kwa kufanikisha mradi huo utakaosaidia kuzuia vifo vya wazazi na watoto hasa wanaozaliwa kabla ya wakati ama chini ya uzito. "Kila mwaka Kanda ya Afrika inapoteza watoto milioni hivyo WHO tutaendelea kuunga mkono jitihada hizi ili kuhakikisha hakuna mtoto ama mzazi anapoteza maisha" amesema Prof. Janabi huku pia akiipongeza Serikali y...