Skip to main content

Posts

Showing posts from October 26, 2015

LUKUVI WA ISMANI NA MGIMWA WA KALENGA WATETEA MAJIMBO YAO

Mgimwa Lukuvi Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ismani, Pudenciana Kisaka amemtangaza Lukuvi Wangimembe William    (CCM)   kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa mwaka 2015-2020 kwa kupata kura 26,119 sawa na asilimia 61 ya waliopiga kura dhidi ya mgombea kupitia Chadema Sosopi Patrick Kapurwa aliyepata kura 15,534 sawa na asilimia 36.18 ya waliopiga kura. Vilevile,  Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kalenga, Pudenciana Kisaka  amemtangaza Geoffrey Mgimwa  (CCM)  kuwa mshindi   wa jimbo hilo kwa mwaka 2015-2020 kwa kupata kura  40,214. Jimbo la Kalenga kura zilizopigwa 56489 na kura halali ni 54,939. Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi sura 343, ya mwaka 2010 inampata mamlaka msimamizi wa majimbo hayo kuwatangaza kuw wabunge kwa mwaka 2015-2020.

UCHAGUZI KURUDIWA KATIKA KITUO CHA IPOGORO 'C' MJINI IRINGA

Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chadema katika Jimbo la Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa (juu ya gari) akiwatumiza mzuka wafuasi wake ili tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) iendelee na mchakato wa kutangaza matokeo ambayo hata hivyo bado hajatangazwa. CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Iringa Mjini kimeyapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Ubunge na Rais jimbo la Iringa Mjini yanayoelekea kukipa ushindi mkubwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Matokeo hayo yameshindwa kutangazwa leo kama ilivyotarajiwa na wafuasi wengi wa chama hicho na wakazi wengine wa jimbo hilo baada ya kutokea wizi wa maboski mawili yaa kura katika kituo cha kupigia kura cha Ipogolo ‘C’, majira ya saa nne usiku, Oktoba 25. Wakisubiri matokeo hayo leo, mamia ya wafuasi wa Chadema walikuwa wamejazana nje ya ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Ahmed Sawa toka saa 12.00 asubuhi hadi 11.00 jioni walipotangaziwa kwamba matokeo hayo hayatatangazwa mpaka kesho wapiga kura...

COSATO CHUMI MBUNGE MTEULE WA MAFINGA MIJINI...!

Mbunge Mteule Jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa Cosato Daudi Chumi akishehekea na wafuasi wake ushindi wa jimbo hilo katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya MUFINDI. Mbunge Mteule Jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa Cosato Daudi Chumi akiwa na mke wake Ester Mbezi akishehekea na wafuasi wake ushindi wa jimbo hilo katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya MUFINDI. Tume ya taifa ya uchaguzi imemtangaza Cosato Daudi Chumi kuwa mshindi wa Jimbo la Mafinga Mjini kwa kushinda kura 18379 asilimia 58 dhidi ya mpinzani waka William Mungai wa Chadema aliyepata kura 12834 - 41%. (Na Mpigapicha Wetu)