Skip to main content

Posts

Showing posts from February 19, 2015

PINDA : TUTAUNGANISHA NGUVU KWA MGOMBEA URAIS ATAKAYE TEULIWA NA CHAMA!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza mwanafunzi wa shule ya  sekondari Kiwere akifanya vitu vyake kwa kushirikiana wanafunzi  wenzake katika maabara ya kemstri  alipotembelea shule hiyo kwa  ajili ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa shuleni. Pinda leo  alikagua ujenzi wa maabara na kufungua nyumba nne za walimu wa shule hiyo zenye uwezo wa kubeba familia nane, halmashauri ya wilaya ya iringa katika jimbo la kalenga.  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua mradi wa umwagiliaji pamoja na mashamba ya wakulima wa mpunga wa kijiji cha magozi, halmashauri ya wilaya iringa jimbo la isimani, akifuatana na  mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza akifuatia na kaimu mkuu wa wilaya ya iringa Gerald Guninita ambaye pia ni DC wa kilolo. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka watanzania hasa wana chama wa chama cha mapinduzi ( CCM)kuwa na subira katika kumpata mwanachama atakayefaa kusimama kugombea urais kupitia CCM mwaka huu.