Skip to main content

Posts

Showing posts from August 29, 2016

JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu. Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao. Msaada ukitolewa. Hapa ni furaha pamoja na watoto hao. Watoto wakipata msaada huo. Watoto wakipokea msaada. Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao. Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao. Na Dotto Mwaibale JESHI la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj Mgulani limetoa msaada wa vyakula na sabuni kwa watoto waishio Makao ya Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini jijini Dar es Salaam. Akizun...

Daladala uso kwa uso na gari dogo

Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa. Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika. Daladala hiloegonga gari namba T 458 CAN. Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo. Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo. Na Dotto Mwaibale MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia. Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika baraba...