Skip to main content

Posts

Showing posts from July 10, 2011

POMBE YA WANZUKI YA BORESHA MAISHA YA KINAMAMA

KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanzisha mradi wa kupika pombe aina ya Wanzuki kwa ajili ya kuwezeshana wenyewe kwa wenyewe. Kikundi hiki cha Upendo kipo katika Mtaa wa Lipinyapinya, Peramiho ‘B’ Wilaya Songea mkoani Ruvuma. Kinywaji baridi cha wanzuki hutengenzwa kwa kutumia maji, majani ya chai, sukari na amila na kusindikwa kwenye chupa mbalimbali zikiwemo za soda, bia na maji. Mweyekiti wa Kikundi  cha Upendo Bi. Asumpta  Luoga alisema kuwa kikundi hiki kilianza tarehe  5 May, 2011 kikiwa na wanachama wachache  kwa mboga  za majani hasa Chinese, na kwa sasa kina jumla ya wanachama 20. “Tulianza kwa kuuza Chinese baada ya kuona kuwa mtaji umekuwa kidogo tukaachana na biashara hiyo na kubuni biashara nyingine japo tulianza kutengeneza pombe ya kiyenyeji aina ya Wanzuki” alisema Bi. Luoga. Pombe hii ya Wanzuki malighafi...