Skip to main content

Posts

Showing posts from April 25, 2017

GARI LA ZIMAMOTO IRINGA LAPATA AJALI LAJERUHI WATANO

Gari la Jeshi la zimamoto na uokoaji la mkoa wa Iringa likiwa limepinduka na kujeruhi watu watano katika kijiji cha Ikengeza, Kata ya Isimani wilayani Iringa, mkoani Iringa juzi.  Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Iringa halina gari la zimamoto baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka na kujeruhi askari wanne wa jeshi hilo akiwemo raia mmoja katika Kijiji cha Ikengeza tarafa ya Isimani wilayani Iringa usiku wakuamkia jana, kilometa tano kutoka barabara kuu ya Iringa-Dodoma.  Akiongea na nipashe jana kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Iringa Kennedy komba alisema askari watatu kati ya wanne wa kikosi cha zimamoto na uokoaji Manispaa ya Iringa walipata ajali ya gari jana usiku saa 4:45 wakati wakielekea kuzima moto kijiji cha Ikengeza.  Alisema raia huyo ambaye alikuwa kwenye gari hilo aliombwa na askari hao ili kuwaongoza kufika katika kijiji hicho lakini hata hivyo gari hilo halikufanikiwa kuzima moto baada ya dereva gari l...