Skip to main content

Posts

Showing posts from December 17, 2012

VIJANA ZAIDI YA 1600 KUAJIRIWA

Na Friday Simbaya KAMPUNI inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya Urani ya Mantra Tanzania Ltd iliyopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imesema itatoa ajira kwa vijana zaidi 1600 kutoka vijiji mbalimbali baada ya kupatiwa kibali cha kuanza kazi ya uchimbaji. Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mjeolojia Mkuu kampuni hiyo Bw. Emmanuel Nyamusika wakati alipokuwa akitoa taarifa mbalimbali kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma (RPC) walipotembelea eneo la mgodi wa madini hayo kwa lengo la kujiridhisha baada ya kupata malalamiko kutoka vijijini vilivyo jirani mgodi huo. Alisema,licha ya kutoa ajira hizo kwa vijana,kampuni hiyo imeshaanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali ya awamu ya nne kwa kuwahamasisha wakazi wa vijiji jirani na mgodi huo kuanzisha vikundi vya kiuchumi na tayari imeshaanza kutoa fedha za kuwawezesha wanavikundi hao kuifanya shughuli za maendeleo kama ufugaji wa kuku wa mayai na nyama. Alisema,lengo la kufanya hivyo ni kutaka wananchi hao kunufa...

MSIMU WA KILIMO

Mkazi wa Peramiho mkoani Ruvuma,Grace Haule akilima shamba  la mahindi nyuma ya nyumba yao jana, ingawa mvua yenywe imekatika kwa muda sasa takriban wiki moja na nusu.