Skip to main content

Posts

Showing posts from June 8, 2016

MAGAZETINI LEO ALHAMISI

TIGO YAMPONGEZA CHRISTIAN BELLA KUTIMIZA MIAKA 10 KATIKA TASNIA YA MUZIKI

Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga akiongea na waandishi (Hawapo pichani )kuhusu udhamini wa Tigo kwenye tamasha la kutimiza miaka 10 ya Christian Bella zilizofanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita katika viwanja vya Escape One kushoto kwake ni Mwimbaji wa mahiri wa dansi nchini Christian Bella .  Msanii wa muziki wa dansi, Christian Bella (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe ya kutimiza miaka kumi katika tasnia ya muziki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita , kushoto kwake ni William Mpinga Meneja Chapa wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo. Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga akimkabidhi simu aina ya Iphone 6 Msanii Christian Bella ikiwa ni kumpongeza kwa kutimiza miaka 10 katika tasnia ya muziki mapema mwisho wa wiki iliyopita ambapo tigo pia walidhamini tamasha hilo 

KIBAHA WALIA UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA

Wananchi wa Mtaa wa Mwambisi wakifua kwa kutumia maji ya mabondeni Wakazi wa Mtaa wa Mwambisi Kata ya Kongowe iliyopo wilayani wakichota maji ya mabondeni kutokana na maji safi na salama katika kata hiyo kutoka mara moja kwa wiki na kusababisha kero na hofu kwa watumiaji wa maji hayo. Picha zote na Elisa Shunda Mmiliki wa Blog ya Shunda Blog,Elisa Shunda, akichota maji kwa ajili ya matumizi ya kuoga Wananchi wa mtaa huo wakielekea katika eneo la Bonde la Miti Mirefu kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kama kufulia nguo,kupikia na kunywa jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa afya yao. NA ELISA SHUNDA,KIBAHA Serikali imeombwa kuingilia kati suala la ukosefu wa upatikanaji wa maji safi katika kata ya Kongowe eneo la Mwambisi ambalo maji yamekuwa yakitoka mara moja kwa wiki na kusababisha wananchi kutumia maji ya mabondeni yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu. Wakizungumza na Raia Tanzania,jana wakazi wa maeneo mbalimbali w...

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HUU

Rais John Magufuli,  RAIS John Magufuli leo amemteua Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji Kiongozi, . Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mchana huu na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu imeeleza “Jaji Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Ally Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.” Kabla ya uteuzi huo, Jaji Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, mkoani Tanga.

MAGAZETINI LEO JUMATANO