Skip to main content

Posts

Showing posts from August 28, 2017

HIZI NDIO MECHI KUBWA ZA WATANI WA JADI BARANI AFRIKA

Na Jumia Travel Tanzania Miongoni mwa matukio yanayosisimua zaidi kwenye mchezo wa soka ni mipambano ya watani wa jadi. Katika nchi nyingi barani Afrika ukiwauliza kwa harakaharaka mashabiki wengi wa soka ni mechi zipi huwa wanazisubiria sana utawasikia wanakutajia michezo kama vile Real Madrid na Barcelona, Manchester United na Manchester City, Inter Milan na AC Milan, Liverpool na Manchester United, Chelsea na Arsenal au Bayern Munich na Borussia Dortmund. Kutokana na umaarufu wa soka la nchi za Ulaya imekuwa ni rahisi kwa mechi zao kufuatiliwa kwa urahisi ukilinganisha na huku Afrika. Lakini hiyo haimaanishi kwamba bara la Afrika nalo halina michezo ya namna hiyo ambayo ikiwa inakaribia homa miongoni mwa mashabiki huwa juu kuliko kawaida. Ukweli ni kwamba mechi za namna ya mifano iliyotajwa hapo juu zipo na zimekuwa zikichezwa kwa miaka mingi tu.kw au pengine inawezekana ukawa unazisikia tu lakini haujui umuhimu uliopo pindi zinapokutana. Jumi...

RODRICK MPOGORO AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA MAKATIBU WA UVCCM MIKOA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI

Naibu katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi ndg; Rodrick mpogoro akifungua Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam. Mwenyekiti wa umoja wa Vijana na mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Ndg:Sadifa Juma khamisi akizungumza katika Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam washiriki wa mafunzo elekezi wakifuatilia mafunzo  mshiriki Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa kirimanjaro ndg; abdulrahim hamid akiuliza swali...

RAIS WA TLS TUNDU LISSU ATANGAZA MGOMO WA SIKU MBILI...

SIKU Moja baada ya Ofisi za IMMMA Advocates zinazomilikiwa na Mawakili Fatma Karume na Lawrence Masha kuungua kwa shambulio la mlipuko wa Mabomu,Rais wa chama cha Mawakili Tanganyika Tundu Antiphas Lissu, amewataka mawakili wote nchini kutokwenda mahakamani siku ya jumanne na jumatano, kuonyesha kupinga vitendo walivyofanyiwa mawakili wenzao wa IMMMA, ambao ofisi yao ilichomwa moto. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hii, Tundu Lissu amesema kitendo hicho kinaingilia uhuru wa wanasheria na taaluma ya sheria, kinahatarisha uhuru wa mahakama na utawala wa sheria kwa ujumla, na kuwataka mawakili walio nchini Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kutoonekana mahakamani kufanya kazi yao. "Baraza la uongozi linawataka wanachama wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria katika mahakama pamoja na mabaraza ya aina zote kati ya siku za jumanne na jumatano ya tar 29 na 30 Agosti 2017, kwa lengo la kuwaunga mkono mawakili wa IMMMA, na kuonyesha k...

ZITTO KABWE AISHIKA PABAYA TENA SERIKALI...

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ameweka wazi kuwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi hususan chakula yanazidi kushuka tofauti na tunavyonunua katika kipindi hiki ambacho nchi inapambana kuingia kwenye uchumi wa viwanda. Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika tathmini ya hali ya uchumi kwenye mauzo, na kusema kuwa anguko kubwa la mauzo tofauti na tunavyonunua, linatufanya kuzidi kuwa tegemezi. “Uagizaji wa bidhaa za chakula kutoka nje umeongezeka kwa 14% ndani ya mwaka mmoja wa Mei 2016 mpaka Mei 2017, ambapo Tanzania ilitumia dola 480 milioni kuagiza vyakula kama sukari, nafaka na mafuta ya mawese. Tumekuwa tegemezi zaidi, tunauza bidhaa kidogo zaidi nje ya nchi, na tunanunua bidhaa zaidi kutoka nje", aliandika Zitto Kabwe. Mbunge Zitto Kabwe aliendelea kuandika kuwa pesa ambayo serikali inapoteza kwa anguko la mauzo ya bidhaa ndani ya miaka miwili ni nyingi, ambayo ingeweza hata kununua ndege 23 za aina ya bomberdier...