Iringa. Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeshauriwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato yatokanayo na vibali vya ujenzi ili kuongeza mapato na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Ushauri huo umetolewa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Sifaeli Kivamba, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026. Kivamba alisema halmashauri inapoteza mapato kutokana na kutosimamia ipasavyo utoaji na matumizi ya vibali vya ujenzi, huku ujenzi ukiendelea katika maeneo mbalimbali bila vibali halali. “Kuna ujenzi unaendelea kila siku lakini wengi hawana vibali, hali ambayo inainyima Serikali mapato. Naomba waheshimiwa madiwani mfuatilie suala hili katika maeneo yenu kwa kuhoji kila anayeendelea na ujenzi kama ana kibali,” alisema Kivamba. Hata hivyo, aliipongeza Baraza la Madiwani kwa kusimamia vyema muda wa mkutano huo uliodumu kwa saa moja na nusu pekee, ikilinganishwa na awali ambapo vikao vilikuwa vikichukua had...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.