Skip to main content

Posts

Showing posts from April 26, 2016

MA DC WATATUA MGOGORO WA MPAKA KWA VIJIJI VYA ILAMBILORE NA ILORE

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Selemani Mzee na Mkuu wa wilaya ya Iringa DC Richard Kasesela walishiriki katika kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji vya Ilambillore (kilichoko Iringa DC ) kijiji cha Ilore kilichoko Kilolo. siku 3 zilizo pita wananchi walitaka kupambana kugombania mipka ambapo walifyeka msitu ambapo ulizua tafrani.

Wananchi wa Kigogo wanufaika na upimaji bure wa afya kutoka Fazel Foundation na TAHMEF

Na Rabi Hume, MoDewjiBlog Kwa kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya usalama wa kiafya, Taasii ya Fazel Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF) wametoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Kigogo, Dar es Salaam. Zoezi hilo lilifanyika Aprili, 23 katika Msikiti wa Al Ghadir uliopo Kigogo Post na jumla ya 352 wanawake wakiwa 150 na wanaumme 202 walipimwa Malaria, Kisukari, Shinikizo la Damu na Upungufu wa Damu mwilini. Kati ya watu hao, watu 38 wameonekana kuwa na Shinikizo la Damu, 36 Upungufu wa Damu, 8 Kisukari na mmoja Maralia ambapo walipata nafasi ya kupatiwa dawa na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali. Aidha kwa mafanikio hayo, Fazel Foundation inawashukuru wote walioshiriki katika huduma hiyo akiwepo Dkt. Mohammed Alloo, Dkt. Sibtain Moledina, Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Salama Pharmaceuticals na Clinicheck Labs, Imam wa msikiti wa Al Ghadir Sheikh Jalala, Msikiti wa Al Gh...

Hospitals braced for walkout as Hunt says doctors' strike must be defeated

Jeremy Hunt and senior ministers have insisted they must win the battle with junior doctors, who are staging a historic walkout that will disrupt services including maternity, accident and emergency and intensive care. Junior doctors to go on all-out strike – Q&A Read more The health secretary dashed any lingering hopes of a last-minute compromise when he told MPs that he was determined to impose the unpopular new contract to help turn the NHS into a seven-day service. The strike is running from 8am to 5pm on Tuesday and Wednesday. A&E and maternity units will be staffed almost entirely by senior consultants as hospitals pull out the stops to ensure patient care is as safe as normal. A very large majority of junior doctors are likely to strike, with only a tiny number expected to defy the picket lines, although the exact figures will be closely scrutinised. In a combative performance in the Commons, Hunt said: “No trade union has the righ...

WAZIRI UMMY MWALIMU AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KWA KUPIMA MALARIA KWA KUTUMIA mRDT

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria. Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watanzania kwa pamoja kuungana kupambana na ugonjwa wa Malaria ili kusaidiana na serikali kutokomeza ugonjwa huo ambao husababisha vifo vya watu wengi nchini. Waziri Ummy ameyesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya Maralia Duniani ambapo huadhimishwa Aprili, 25 ya kila mwaka na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu ili kutokomeza ugonjwa huo. “Msisitizo mkubwa wa Wizara yangu ni kwa wananchi na wadau wote kuona umuhimu na kutoa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malar...
Paulina Mgeni ndio Miss Utalii Mkoa wa Iringa mwaka 2013 mpaka sasa kabla mashindano hayo hayaja simamishwa; ila kwasasa anafanya kazi za mitindo akiwa kama Mwanamitindo (Model), lakini anahitaji meneja wa kusimamia kazi zake hizo za Urembo (Modeling). Paulina Mgeni ni Mwanamitindo (Model) anaefanya kazi za urembo na maonesho ya mitindo kwa kujitegemea yeye mwenyewe hayupo chini ya kampuni yoyote wala chini ya lebo ya mtu yeyete, japokua amekuwa akifanya shoo nyingi kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni na wabuni mbalili, kwasasa anatafuta Meneja wa kuwa anamsimamia kazi zake. Mwaka 2013 Paulina alikuwa Miss Utalii mkoa wa Iringa, akafanikiwa kuingia ngazi ya Taifa na kupata tuzo ya the Best Model of Tanzania, pamoja na kuwa Balozi wa models Tanzania; amefanikiwakufanya maonesho (shows) mbali mbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania. Mwanamitindo Paulina Mgeni akiwa katika pozi. Paulina amefanya kazi na wabunifu mbali mbali (designers) kama vile Asia Ida...

Kilombero Community Charitable Trust wajenga darasa

Mkurugenzi Mtendaji wa Kilombero Sugar Mark Bainbridge akiwaongoza Wazazi na wafanyakazi wa Kilombero Sugar kukagua darasa katika shule ya msingi Muungano lililojengwa kwa ufadhili wa chama cha kusaidia jamii cha Kilombero Community Charitable Trust (KCCT). Hafla hiyo ilifanyika Kilombero mwishoni mwa wiki. Mkurugenzi mtendaji wa Kilombero Sugar Mark Bainbridge akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi ya Muungano mbele ya darasa la awali lililojengwa kwa ufadhili wa chama cha kusaidia jamii cha Kilombero Community Charitable Trust (KCCT) Hafla hiyo ilifanyika Kilombero mwishoni mwa wiki. Mwakilishi wa Kilombero Sugar Joseph Rugaimukamu akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Muungano baada ya kukabidhiwa madawati na chama cha kusaidia jamii cha Kilombero Community Charitable Trust (KCCT), hafla hiyo ya kukabidhi ilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.  ****************** Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kimewekeza zaidi ...