Skip to main content

Posts

Showing posts from November 9, 2015

Fahamu jinsi RecruitMe inavyoweza kukupa ujuzi utakaokusaidia kupata kazi

Ujuzi, katika soko la ajira ni mali ambayo inahitaji matengenezo na uboreshaji. Kama mali nyingine yoyote, matumizi yake bora, hukuzalishia zaidi. Sababu nyingi zimetolewa katika kipindi cha miaka mingi kwamba kuna utofauti wa wazi baina ya mtu mwenye elimu aliyeko kazini na mwenye elimu bila kazi. Utofauti huo ni jinsi ujuzi wa watu hao wawili unavyotumika. Vijana wengi wa Tanzania wana ujuzi waliopata kutokana na mafunzo mbalimbali, lakini baadhi yao kushindwa kutumia ujuzi walionao. Sababu pekee inayosababisha hili ni; mahitaji ya ujuzi katika soko la ajira hayako sambamba na ujuzi utolewao. Matokeo yake ni vijana kujikuta kwenye sintofahamu iliyosababishwa na mgongano wa kiujuzi. Ushindani mkubwa katika soko la ajira duniani ni kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA ambayo imechukua nafasi kubwa ya ajira za watu, na kama ajira inahitajika basi mtu ni lazima uwe na ujuzi maalumu. Mwalimu mjini Arusha mwenye ujuzi wa TEHAMA ana nafasi kubwa ya kupata ajira kuliko yule as...

MAGAZETI LEO JUMANNE NA SIMBAYABLOG

UJUMBE WA MKURUGENZI MKUU WA UNESCO KUHUSIANA NA SIKU YA SAYANSI YA DUNIANI

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova. Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Lenye makao yake makuu jijini Paris, Ufaransa kupitia Mkurugenzi wake Mkuu limetoa ripoti ya ujumbe wake kuelekea siku ya Sayansi Duniani kwa amani inayotarajia kuadhimishwa leo hii Novemba 10, Duniani kote. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO , Bi Irina Bokova, katika ujumbe wake, juu ya maadhimisho ya leo ameweza kugusia mambo mbalimbali: "Hii Siku ya Sayansi Duniani kwa Amani na Maendeleo imekuja miezi miwili baada ya makubaliano ya Agenda 2030 ya maendeleo endelevu. Ajenda hii mpya inajumuisha maono mapya kwa binadamu, kwa dunia, kwa amani , kwa miaka 15 ijayo na sayansi inasimamia katika moyo wake kama kichocheo cha mageuzi chanya na maendeleo. Serikali zote kwa ujumla zinatambua leo nguvu ya sayansi ya kutoa majibu muhimu kwa usimamizi mzuri wa maji, kwa ajili ya hifadhi na matumizi endelevu ya bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe hai, ili ...

CHEKI.CO.TZ ADVICES ON STAYING ALERT WHEN SHOPPING ONLINE

Buying anything online is a tough gig – you’re behind your laptop gazing longingly at potential dream purchases, you never know who is waiting eagerly for your hard earned cash to fall into their pockets. While there are many legitimate sellers online, there are few but very dangerous fraudulent online sellers that makes online purchases a bit challenging. Popular online fraud includes lotteries and sweepstake scams, dating scams, Nigerian Email scams and money transfer scams but there are many scammers coming up with new methods every day. But just like on the traditional business arena, there are a few things you should pay good mind to before you head to the proverbial checkout, especially when it comes to important purchases like a car.  When you transact online, who are you buying from is as important as what you buy. The possibility that you’ll be able to give a 100% certain answer to this question is a bit of a myth. But when you are buying a car, for the...

BABU SEYA NA MWANAE WATINGA MBELE YA MAHAKAMA YA HAKI ZA BINAADAMU

Mwanamuziki, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, wametua katika Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AFCPHR) Arusha. Wanamuziki hao wamekata rufaa dhidi ya adhabu waliyohukumiwa mwaka 2004 ya kutumikia kifungo cha maisha gerezani. Kupitia shauri lao lililowasilishwa mahakamani na kupewa namba 006/ 2015, wanaiomba Mahakama ya Afrika kutoa uamuzi kuwa haki zao zilivunjwa. Kwa sababu hiyo wanaomba waachiwe huru na kulipwa fidia. Katika shauri hilo pia wameomba wawezeshwe kupata msaada wa sheria na. Pia wanataka Mahakama hiyo iteue wataalamu watakaotoa ufafanuzi wa hoja za kesi yao na kuisaidia kufikia wajibu wake. Miongoni mwa hoja za walalamikaji hao zilizowasilishwa mahakamani hapo ni pamoja na kwamba mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki,. Vilevile wanadai hati ya mashtaka dhidi yao ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa kutayarisha utetezi wa...

MAHAFALI YA MTOTO WETU REGINA SIMBAYA

The Celebrating the form four graduation of our daughter Regina  Kenneth Simbay a  at Joyland Girls secondary School in Same, Kilimanjaro region few weeks ago. Kulia ni baba mzazi wa Regina Kenneth Simbaya, baba mdogo wa regina Moses Allan Adam na mdogo wake Frank  Simbaya. Hongera Regina kwa hatua uliofikia.