Skip to main content

Posts

Showing posts from December 25, 2016

NYAMA YA NG'OMBE MJINI IRINGA YAPANDA SIKUKUU YA KRISMASI

Baadhi ya wateja wakiwa katika mmoja ya mabucha ya nyama ya ng’ombe leo mjini Iringa, mkoani Iringa wakati huu wa kusherehekea siku kuu ya Noeli. (Picha na Friday Simbaya) IRINGA: Wakristo duniani kote wanasherehekea Sikukuu ya Krismasi, jana msongamano katika soko la Manispaa ya Iringa na mitaa maarufu ya Mashine tatu na M iyomboni iliongezeka, huku baadhi ya bidhaa zinazotumika kwenye sikukuu, ikiwemo nyama, zikiwa zimepanda bei. Wakazi wa mjini Iringa wamesema bei ya nyama ya ng’ombe imepanda katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi. Walisema kuwa nyama ya ng’ombe imepanda kutoka shilingi elfi sita hadi kufikia shilingi elfu sita na mia tano kwa kilo moja. SIMBAYABLOG ilIshuhudia baadhi ya mabucha ya nyama ya ng’ombe yakiwa yamefurika wateja katika maeneo mbalimbali ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa leo asubuhi. Elizabeth Kadaga ni mkazi wa Frelimo, Manispaa ya Iringa alisema kuwa wafanyabiashara huwa wanatumia mwanya wa siku k...

WAKRISTO WALIVYOSHIRIKI IBADA YA MKESHA WA KRISMASI JIJINI DAR ES SALAAM

Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Violet Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam. Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam. Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi. Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo. Kwaya ya Vijana ya KKKT usharika wa Azania Front ikitoa burudani. Kwaya ya vijana ya KKKT Usharika wa Azania Front ikiendelea kutoa burudani. Watoto wakishiriki ibada katika Kanisa la KKKT la Azania Front Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akimsalimia muumini wa kanisa hilo, Violet Njau aliyekuwa ameongoza na familia yake. wau...