Skip to main content

Posts

Showing posts from February 26, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI

TAMWA YASIKITISHWA KESI ZA UBAKAJI/ULAWITI KWA WATOTO KUTOHUKUMIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(katikati) akizungumzia mbele ya waandish wa habari (hawapo pichani) ni kwa jinsi gani wamepata malalamiko kutoka kwa familia zinazofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi za mahakama, polisi na baadhi ya hospitali hapa nchini. Mratibu wa Kituo cha Usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa wakilaani vikali ucheleweshwaji na upotoshaji wa kesi za vitendo vya ukatili. Mtoto akitoa ushaidi ni kwa jinsi gani alivyofanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia. Mwanasheria wa TAWLA, Mary Richard (wa kwanza kulia) akizungumza ni kwa jinsi gani wanavyowasaidia wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia leo katika mkutano na waandishi wa habari leo. Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini. Chama cha Wanahabari wanawake nchini Tanzania(TAMWA) kimelaani vikali ...

MTAMBUE KIJANA WA KITANZANIA DESMOND ANDREW ALIYEANZISHA KAMPUNI YA MAWASILIANO YA CW NET

Kijana wa Kitanzania Desmond Andrew alimeanzisha kampuni ya Mawasiliano ya CW Net ambayo inatengeneza Power Bank, Smart Bracelet na Modem. Hakika Tanzania kuna vijana wengi kama Desmond Andrew lakini tatizo kubwa linalowakabili ni upatikanaji wa mtaji wa kuendeleaza vipaji vyao. Mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya Mawasiliano ya CW Net akimtoa ufafanuzi Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) kuhusu Smart Bracelet na kazi zake katika maonesho yaliyoandaliwa na shirika la Viwango nchini Tanzania(TBS) yanayoendelea katika ukumbi wa Mlimani Cityjijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) akiuliza swali mara alipotembelea banda la CW Net maonesho ya Makampuni ya Kitanzania yanayotoa bidhaa yenye viwango vya kutosha hapa nchini. Smart Bracelet hiki ni kifaa mojawapo kinachotengenezwa na kampuni ya Mawasiliano ya CW Net ambacho kifaa hicho kinahesabu hatua ambazo mtu ametembea nani k...

ACTION AID NA NORAD WAZINDUA MRADI WA KUSAIDIA UBORESHWAJI ELIMU NCHINI

Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).(Picha na Modewjiblog ). Katika kusaidia uboreshwaji wa elimu ya Tanzania, Shirika la Kimataifa la ActionAid kwa kushirikiana na serikali ya Norway kupitia Wakala wa Maendeleo na Ushirikiano (NORAD) wamezindua mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization). Akielezea kuhusu mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama alisema mradi huo unataraji kusaidia uboreshwa wa elimu nchini na zaidi maeneo ya vijijini sehemu ambapo zimekuwa zikionekana kuwa nyuma kielemu. Alisema ili kupatikana kwa elimu bora kunahitajika uwekezaji wa kuboresha elimu kwa maeneo yote yanayohusika n...