Skip to main content

Posts

Showing posts from April 23, 2015

KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA HASSAN MTENGA AENDELEA KUVURUNGA MIPANGO YA WAPINZANI KATIKA JIMBO LA ISMANI

katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwahutubia wananchi wa tarafa ya pawaga. katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akijibu maswali ya wananchi wa tarafa ya pawaga. katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwapa vifaa vya michezo wananchi wa tarafa ya pawaga na fredy mgunda,pawaga katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa hassani mtenga amewataka wananchi wa tarafa ya pawaga katika  jimbo la isimani kuendelea kumwamini mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa anawatendea  haki kwa kuwaletea maendeleo.

KITABU CHA 'THE 7 HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE' CHAZINDULIWA UPYA KWA LUGHA YA KISWAHILI

Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia) akimwonyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog ). Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto) akipitia kurasa mbalimbali za kitabu hicho kabla ya uzinduzi rasmi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege.