Skip to main content

Posts

Showing posts from November 27, 2013

TATIZO LA MIMBA KWA WANAFUNZI PERAMIHO TISHIO

Na Friday Simbaya, Songea Asumpta Magunga mwenye miaka kumi na saba (17) wa Kijiji cha Peramiho, Wilaya ya Songea (V) mkoani Ruvuma amezaa mtoto asiyekuwa na ngozi tumboni, yaani amezaliwa na viungo vyote vya ndani vinaonekana wazi   kwa kitaalamu wanaita (congenital malfunction) katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho. Magunga ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili Shule ya Sekondari Namihoro, willayani Songea Vijijini mkoani Ruvuma ni mkazi wa mtaa wa Lihangano katika kijiji cha Peramiho alijifungua mtoto bila ngozi ya tumboni, lakini bahati mbaya mtoto huyo hakuishi muda mrefu alifariki dunia Jumapili tarehe 24 Novemba mwaka huu. Nilipopata taarifa kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wa ajabu mwenye kuzaliwa na viungo vya ndani vikiwa nje nilichukuwa kamera ya ofisini na kukimbia mara moja hospitalini kupata picha na maelezo kidogo kuhusiana na tukio lenyewe. Nilipofika pale hospitali nilikwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Muuguzi Mkuu, Romanus Mgimba am...