Skip to main content

Posts

Showing posts from December 15, 2015

UNCDF YATOA BILIONI 2.4/- KUSAIDIA MIRADI 6 YA MIUNDOMBINU

Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika akizungumza na wageni waalikwa wakati wa makabidhiano ya misaada kwa miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na UNCDF Tanzania. Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba akisoma hotuba yake wakati wa kukabidhi hundi kwa mashirika binafsi na ya umma kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo. Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (katikati) akimkabidhi hundi bilioni moja na milioni sabini (1,070,000,000) Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha, Bi. Jennifa C. Omolo (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika. Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bw. Jeshi Godfrey Lupembe (kushoto) akikabidhiwa hundi ya shilingi milioni mia tano na tisa (509,000,000/=) na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa...

ZIARA YA WAZIRI WA MADINI PROFESA MUHONGO MKOANI IRINGA

Waziri wa madini nchini Profesa Sospeter Muhongo aliye wasili mkoani Iringa Siku ya Jana na kutembelea vijiji kadhaa mkoani humo. Muhongo amewasili Iringa akitokea Pangani mkoani tanga lengo ni kuangalia hali ya vyanzo vya maji vinavyozalisha Umeme Akipokewa na mwenyeji wake ambaye ni mkuu Wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela na kutembezwa baadhi ya vijiji vilivyopo Pawaga na Isiman panapo unganisha bwawa la mtera Kwa mujibu Wa Kasesela amesema hali ya bwawa la mtera ni mbaya kwani maji yamekauka na kusababisha ukaukaji Wa maji Hali hiyo imemfanya Pr. Muongo kuagiza kufanyika kwa kikao cha wadau Wa maji, misitu, Tanapa, wavuvi nk mapema kutafuta suluhisho la janga hilo Kasesela amesema atafanya kikao hicho mapema Juma tatu ya wiki ijayo ofisini kwake mawelewele na baadae kuelekea mtera.

DC MAKONDA, MBUNGE SAED KUBENEA WATIFUANA MBELE YA WANANCHI

MBUNGE wa jimbo la Ubunge jijini Dar es Salaam, (CHADEMA), Saed Kubenea (mwenye shati jeusi kulia), akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (mwenye t-shirt ya michirizi), huku wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha ..... kilichoko eneo la EPZ, Ubungo jijini Dar es Salaam, Desemba 14, 2015.   Wakubwa hao wawili walianza kulumbana baada ya mbunge Saed Kubenea kuitwa na wafanyakazi hao kufuatia mgogoro wa malipo ya mishahara ambayo wafanyakazi wanadai ni midogo haiendani na uhalisia wa kazi wanazozfanya.  Wakati mbunge huyo aiendelea kusikiliza kilio cha wafanyakazi hao ambao kimsingi wako kwenye eneo lake la uwakilishi, Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni ambaye eneo hilo liko chini ya himaya yake, naye aliwsili ili kujua nini kimetokea.  Hata hivyo, DC Makonda aliubeba mgogoro huo na kumuweka kando mbunge huyo, hali iliyozua tafrani miongoni mwa wawili hao, baada ya vuta ni kuvute, mbele ya wananchi, hatimaye Mkuu wa Wilya alitumia ...

MAGAZETINI LEO JUMANNE