Iringa. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele, amewataka wasimamizi wa uchaguzi nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria za uchaguzi na kanuni zake, akisisitiza kuwa hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea bali kwa kufuata maelekezo ya Tume. Jaji Mwambegele ametoa wito huo Januari 24, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi ngazi ya jimbo na kata, maafisa uchaguzi, maafisa ununuzi pamoja na wahasibu. Mafunzo hayo yanafanyika kuanzia Januari 24 hadi 26, 2026. Akizungumza katika hafla hiyo, amewapongeza wajumbe wa Tume pamoja na waratibu wa uchaguzi wa Mikoa ya Songwe na Ruvuma kwa uteuzi wao, akisema umezingatia weledi, haki, uwazi na matakwa ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Amesema matarajio ya Tume ni kuona chaguzi zinaendeshwa kwa uadilifu wa hali ya juu, huku aki...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.