Na Friday Simbaya, Ludewa WAKATI Taifa likishehekea mafanikio ya kuudhibiti ugonjwa hatari wa Maralia kwa kugawa vyandarua kwa mama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka mitano Mkoani Iringa bado vyandarua havitoshi, lakini vilivyopo vinatumika kujifunika kama blanketi kujikinga na baridi imefahamika. Hayo yalithibitika hivi karibuni katika kijiji cha Mbwila Kata ya Luana Ludewa Mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria kimkoa ambapo mkuu wa wilaya ya Ludewa Bi Georgina Bundalla alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo kama mgeni rasmi. Desmola Salo (37) aliliambia gazeti hili kuwa vyandarua vinavyotolewa na serikali havitoshi. “” mimi mwenyewe pale nyumbani ninayo familia ya watoto watano, lakini tunacho chandarua kimoja tu ambacho tunakitumia mimi na mume wangu huku watoto wakilala bila chandarua.”” Alilalamika Bi Desmola Kwa upande wake Bi Evelina Haule (65) na Pendo Kayombo wao walikiri kupokea vyandarua vyenye dawa kutoka kwa mawakala wa mabadiliko katika jam...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.