Lawrence Masha na Friday Simbaya leo Dodoma (Picha na Chris Jr Simbaya) Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewachagua wajumbe 7 wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania huku wagombea wawili wa CHADEMA wakipigiwa kura za ‘HAPANA’ na hivyo kushindwa kupitishwa. Wagombea hao wa CHADEMA ni Lawrence Masha na Ezekiel Wenje, ambao pia waliungana na wagombea wengine wote kujieleza mbele ya wabunge kabla ya zoezi la upigaji kura. Kwa upande wa CCM, walioshinda ni 1. Fancy Nkuhi 2. Happiness Legiko 3. Maryam Ussi Yahya 4. Dkt Abdullah Makame 5. Dkt Ngwaru Maghembe 6. Alhaj Adam Kimbisa CUF iliyokuwa na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo Awali palitokea mabishano ya kikanuni juu ya wagombea wa CHADEMA yaliyosabaishwa na chama hicho kuweka wagombea wawili pekee wakati nafasi kwa ajili ya chama hicho zikiwa mbili pia. Baadhi ya wabunge walitaka Spika a...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.