Skip to main content

Posts

Showing posts from April 28, 2016

WWF WAFADHILI MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI WILAYA YA IRINGA

Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Joachim Mshana akisoma matatizo yaliyopo katika kijiji cha Makatapola Kata ya Migoli tarafa ya Isimani kwa mujibu wa tathmini zilizofanyika wa wa PRA wakati wa Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Makatapola jana. Mrasimu Ramani (Cartographer)  wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Geoffrey Mwanga akisoma mapendekezo ya sheria ndogo za kusimamia mpango shirikishi jamii wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji cha Makatapola Kata ya Migoli tarafa ya Isimani, zilizotayarishwa  na kamati ya matumizi bora ya ardhi ya kijiji cha Makatapola, na kupishwa jana na halmashauri ya kijiji na mkutano mkuu wa kijiji. Mpango umefadhiliwa na WWF na halmashauri ya wilaya ya Iringa.  Mkazi mmoja wa kijiji cha Makatapola Kata ya Migoli tarafa ya Isimani akipiga kengele kwa ajili ya kukaribisha wananchi katika mkutano mkuu wa kijiji hicho. Afisa Mipango miji na vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Zahoro Mwalon...