Skip to main content

Posts

Showing posts from May 10, 2017

SHIRIKA LA WOTESAWA LAZIDI KUSAMBAZA ELIMU YA KUTETEA HAKI ZA WATOTO WAFANYAKAZI

Mwanasheria na Msimamizi wa Mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini Tanzania, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina kwa Viongozi wa serikali za mitaa kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza. Semina hiyo ya siku tatu, kuanzia jana Mei 09 imewashirikisha Madiwani, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, Wenyeviti wa Mitaa na dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kusaidia kutetea na kulinda maslahi ya mtoto mfanyakazi wa nyumbani na kumuepusha na utumikishwaji wa kazi ngumu na maslahi duni. #BMGHabari Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina hiyo ambapo pia ameelezea juu ya umuhimu wa viongozi hao kuitambua Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 14 kuajiriwa huku wale walio juu ya umri huo wakipaswa kuajiriwa kufanya kazi zisizo hatarishi. ...

DOROTHY SEMU ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU ACT WAZALENDO

KAMATI Kuu ya Act Wazalendo imemuidhinisha Ndugu Dorothy Jonas Semu(pichani), kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo. Kabla ya uteuzi huu Ndugu Dorothy Semu amewahi kushika nafasi za ukatibu wa Kamati za Sera, Mipango na Utafiti na Kamati ya Fedha na Miradi. Kwa mujibu wa Kiongozi wa ACT-Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe, kupitiaukurasa wake wa Facebook amesema, Ndugu Dorothy Semu ametoa mchango mkubwa kwa chama hasa kwenye uandaaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2015 na masuala mengi ya kiutafiti juu ya sera na mikakati ya Chama. Ndugu Semu ni mtaalamu wa masuala ya Fiziotherapia mwenye shahada mbili za eneo hilo kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, Afrika ya Kusini. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 wa kufanya kazi kwenye nafasi mbalimbali serikalini na kwenye Asasi za kiraia ikiwemo Mratibu wa kuzuia ulemavu kwenye Programu ya Taifa ya Kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma. Tunamtakia kila la heri Ndugu Dorothy Semu kwenye utekelezaji wa majukumu yake.

RAIS MAGUFULI AWAPA MAGARI YA WAGONJWA WABUNGE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa magari mapya matatu ya kubebea wagonjwa kwa Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasaidia wananchi wa maeneo yao ya ubunge. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amekabidhi magari hayo aina ya Land Cruiser Hardtop kwa niaba ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoa wa Rukwa Mhe. Ally Keissy, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa waTabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga. Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Balozi Kijazi amesema Mhe. Rais Magufuli ametoa magari hayo baada ya kuguswa na kilio cha muda mrefu cha Wabunge hao waliokuwa wakiomba wananchi wao wapatiwe magari ya wagonjwa. “Mhe. Rais ameamua kuwakabidhi nyinyi haya magari kutokana na vilio vyenu ambavyo amekuwa akivisikia mara kwa mara, Mhe. Keissy umekuwa hata ukitafuta miadi ya kuja kumuona Mhe. Rais kwa suala hili, Waheshimiwa Wab...

ZIMWI LA AJALI LAZIDI KULITESA TAIFA

Basi la Ally's lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora limegongana na Coaster ya Isanzu uso kwa uso iliyokuwa linaelekea Mwanza kutoka Kahama Ajali imetokea saa mbili asubuhi eneo la Samuye barabara ya Shinyanga.Hali ya dereva wa Coaster ya Isanzu si nzuri. Kamanda wa polisi mkoani hapa, Muliro Jumanne amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya Ally's kuwa kwenye mwendo kasi. Jumanne amesema kuwa abiria waliokuwa kwenye magari hayo ni zaidi ya 70 lakini waliojeruhiwa ni 35 ambao ndiyo wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga. Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk Rashid Mfaume amesema amepokea majeruhi 35 wa ajali hiyo wakiwemo watoto wawili na kwamba kati ya majeruhi hao wenye hali mbaya ni wawili.

BUNGE LATHIBITISHA KUPATA MAJINA KUWANIA UBUNGE EALA KUTOKA CHADEMA

1.Tarehe 4 Aprili, 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya Uchaguzi wa kuwachagua Wajumbe Tisa (9) wa Bunge la Afrika Mashariki watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo. Katika Uchaguzi huo, Wajumbe Sita (6) kutoka Chama cha Mapinduzi na Mjumbe mmoja (1) kutoka Chama cha Wananchi (CUF) walichaguliwa. Wagombea wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)walikosa kura za kutosha kuwapatia ushindi. 2.Hivyo, Bunge linapaswa kufanya uchaguzi kwa mara ya pili ili kuwapata wawakilishi Wawili (2) kutoka katika Kundi la Vyama vya Upinzani ambapo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho chenye hakiya kujaza nafasihizo. 3.Katika mazingira hayo na kwa kuzingatia masharti ya Sheria na Kanuni zinazotawala Uchaguzi huo, na kwa mamlaka niliyonayo kama Msimamizi wa Uchaguzi nilitoa TAARIFA ya Siku ya Uteuzi na Siku ya Uchaguzi kwenye Gazeti la Serikali Na. 537 la tarehe 21Aprili,2017. Taarifa hiyo ilitaja Sik...