Skip to main content

Posts

Showing posts from January 29, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI

Askari polisi auawa kwa kupigwa risasi

Askari polisi Nobart Chacha (25) Wilayani Mlele Katavi ameuawa kwa kupigwa risasi akituhumiwa kupora mali za mfanyabiashara wa madini kwa kutumia silaha za jadi. Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi amesema kuwa askari huyo aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani na mgongoni. Chanzo: East African Radio

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAFUTA KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI

Kulia ni Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza. Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba  25 mwaka jana, katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na  aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM  Christopher Ryoba Kangoye. Katika kesi hiyo,  wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.John Heche  (Chadema), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria  Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba Mahakama kutengua matokeo  ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki. Baada ya Mahakama  hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua  kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 201...