Skip to main content

Posts

Showing posts from March 31, 2018

PAROKIA YA MTANDIKA KUSHEREHEKEA PASAKA KWA MWANGA

Meneja Selebu Rocks Spring Water Ltd Edgar Lamba (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya umeme jua (solar panel kits) kwa Paroko Fr. Silvanus Ndazi wa Parokia ya Mtandika, Jimbo Katoliki Iringa jana.   KILOLO: Parokia ya Mtandika katika Jimbo Katoliki Iringa wilayani Kilolo mkoani Iringa itasherehekea Siku Kuu ya Pasaka kwa mwanga baada ya kupata msaada wa umeme wa nishati ya jua (solar panel kits) kutoka Selebu Rocks Spring Water Ltd Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Msaada huo wenye thamani shilingi milioni 6.9 ni mchango kutoka kwa mkurugenzi na mfanyabiashara mkongwe Mzee John Lamba wa Kiwanda cha maji wilayani kilolo, mkoani Iringa. Akizungumza jana wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya umeme wa jua, Meneja Selebu Rocks Spring Water Ltd Edgar Lamba kwa niaba ya mkurugenzi na mfanyabiashara mkongwe Mzee John Lamba alisema kuwa wamesukumwa kutoa vifaa hivyo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za kiroho nyakati zote na kuzingatia kuwa Parokia ya Mtand...