Skip to main content

Posts

Showing posts from June 12, 2016

WANAWAKE WA KANISA LA MORAVIAN MTONI KIJICHI KUFANYA MAOMBI MAKUBWA YA KUJIOMBEA NA TAIFA

Wanawake wa Kanisa la Moravian Usharika wa Mtoni Kijichi wakiwa mbele ya kanisa lao Dar es Salaam leo asubuhi. Wanawake hao Julai 10 mwaka huu wanatarajia kufanya maombi ya kuwaombea wanawake wote nchini, familia zao pamoja na Taifa kwa ujumla. Na Dotto Mwaibale WANAWAKE wa Kanisa la Moravian Usharika wa Mtoni Kijichi wanarajia kufanya maombi makubwa kwa ajili ya wanawake nchini, familia zao pamoja na taifa kwa ujumla yenye lengo ya kumshuru mwenyezi mungu. Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Mratibu wa tukio hilo Mwalimu Mary Anyitike alisema lengo la maombi hayo ambayo ni rami ni kumshukuru mungu kwa kuzaliwa wanawake. Anyitke alisema maombi hayo yatafanyika katika kanisa hilo Julai 10, mwaka huu saa tatu asubuhi ambapo aliwaomba wanawake wote bila ya kujali dini na madhehebu yao kujitokeza kushiriki maombi hayo ambayo yapo kwa ajili yao. "Maombi haya ni muhimu kwetu na familia zetu na kauli mbiu yetu ni wanawake ni jeshi kubw...

ZITTO KABWE AJILIPUA TENA BUNGENI,AWALIZA WABUNGE

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo amekoleza moto wa wabunge kukatwa kodi katika fedha za kiinua mgogo, anaandika Dany Tibason. Wakati hayo yakifanyika, Serikali ya Rais John Magufuli imewang’oa wabunge wa viti maalumu kushiriki kwenye Kamati za Fedha na Mipango za Halmashauri. Jumatano wiki hii serikali ilisoma bajeti yake ya Sh. 29. 52 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17, sehemu ya bajeti hiyo ilionekana kukera wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Mheshimiwa spika, natangaza kufuta msamaha wa kodi ya mapato kwenye malipo ya kiinua mgongo kinacholipwa kwa wabunge kila mwisho wa muhula wa miaka mitano ili kujenga misingi ya usawa na haki katika utoaji wa kodi kwa kila mtu anayestahili kulipa kodi,” alisema Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango. Kutokana na mpango huo wa serikali kutoza kodi katika kiinua mgongo cha wabunge na kuzua zogo kwa wabunge wa CCM, Zitto amesema, ni vema serikali ikafanya hivyo ili kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi...

JUKWAA LA KATIBA WAANZA KUUFUFUA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Baada ya kimya cha muda mrefu kuhusu sakata la Kupatikana kwa katiba Mpya Hatimaye jukwaa la katiba Tanzania wametangaza Rasmi kurejesha mchakato huo upya ili kuamsha uwezekano wa Serikali kuanza tena mchakato huo ambao uneonekana kusahaulika na wahusika. Mwenyekiti wa Jukwaa la katia Tanzania DEUS KIBAMBA amesema kuwa wamemua kusaidia kuanzisha ambapo wameanza kampeni mpya inayolenga kufufua mchakato wa katiba mpya baada ya kugundua mchakato huo ulijisimamisha wenyewe na sasa unasubiriwa uanze tena wenyewe

Zambia plans to have sub-Saharan Africa’s cheapest electricity using solar power

LOOK TO THE SUN Lake Kariba is drying up, and so is Zambia's electricity supply. (Reuters/Philimon Bulawayo)  Disappointed by hydroelectric power reduced by drought, Zambia is turning to the sun. The landlocked country plans to build two solar projects that will charge the lowest tariffs in sub-Saharan Africa, according to the Zambian Industrial Development Corporation . Solar power development comes as Lake Kariba , the main source of Zambia’s electricity, is at a just 12% of its capacity . The world’s largest man-made lake lies on the Zambezi River between the Zambian and Zimbabwean border and produces 600MW and 750MW for the two countries, respectively. The two solar projects will provide electricity priced at 6.02c/kWh and 7.84c/kWh, respectively. Those prices will remain fixed for 25 years, the corporation said in a statement. Zambians using over 300kWh in their homes pay about 51c/kWh on the current energy tariffs with a standard 31c/kWh for co...

MKOA WA IRINGA UNA WATUMISHI HEWA 169

Mkoa wa Iringa iliunda timu ya wataalam kwa ajili ya kupita katika Hospitali Teule zote za Wilaya na kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kuendelea kubaini iwapo wapo watumishi hewa ambao hawakubainishwa katika zoezi la awali.  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa timu niliyounda imekamilisha kazi yake tarehe 07/06/2016 na kunikabidhi taarifa yake. Kwa ufupi taarifa hiyo imebainisha masuala mbalimbali. Akiongea na waandishi wa habari jana alisema kuna watumishi hewa 169 katika Halmashauri ambao wamekuwa wakipokea mishahara pasipo kustahili kutokana na utoro, kustaafu na kufariki.  Aidha, alisema kuwa upotevu wa fedha kutokana na ulipaji wa mishahara isivyostahili umeisababishia Serikali hasara ya shilingi Milioni 364,028,910.80.  Timu hiyo pia imebaini kuwa, katika Hospitali Teule ya Ilula inayotoa huduma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo lipo tatizo la fedha za mishahara isiyolipwa inayofikia kiasi cha Shilingi Milioni 151,...