IRINGA: Serikali ya Kijiji cha Ihemi imetakiwa kufanya ulinzi shirikishi kulinda chanzo cha maji cha Ihemi ili kiendelee kutiririsha maji muda wote. Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa kikosi kazi namba tatu cha kunusuru ikolojia ya bonde la mto Ruaha mkuu ili liweze kurudi katika hali yake ya kawaida ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu jana katika kijiji cha Ihemi kilichopo katika kata ya Ifunda wilayani Iringa. Ayubu alisema “serikali ya kijiji cha Ihemi inawajibu wa kulinda chanzo cha maji hiki cha Ihemi. Tena ulinzi huu lazima uwe shirikishi ukihusisha wanufaika wote, hasa wakulima na wafugaji”. Aliongeza kuwa mifugo imekuwa ikilishwa katika chanzo hicho cha maji na kupiga marufuku utaratibu huo wa kulisha mifugo katika chanzo hicho. Aidha, aliitaka Halmashauri ya wilaya ya Iringa kutoa ushauri wa kitaalamu katika kutatua changamoto za kiuhifadhi kwa vijiji vyote vinavyozunguka vyanzo vya maji wilayani humo. “Halmashauri ya wilaya ya Iringa nyie...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.