Skip to main content

Posts

Showing posts from December 5, 2017

MEYA WA MANISPAA YA IRINGA: MSITUPE TAKA OVYO

WANANCHI wa Manispaa ya Iringa Mkoani humo wametakiwa kutotupa taka ovyo na badala yake wahifadhi taka hizo kwenye vyombo maalumu vya kuwekea taka. Kauli hiyo imetolewa jana na Meya wa manispaa ya Iringa Alex kimbe wakati akipokea msaada wa mapipa 40 ya kuhifadhia taka kutoka kwa kampuni ya Zanzibar and Nyihita ya mazingira. Alisema pamoja na kuwa manispaa hiyo imekuwa ikishika nafasi ya kwanza hadi tatu za kuwa safi kitaifa lakini bado kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakitupa taka ovyo,hivyo lazima wahakikishe wanatupa taka kwenye vyombo husika. Kimbe alisema pamoja na kuwa vyombo vya kutupiataka ni vichache lakini kila mmoja akalichukulia jambo la usafi ni la kwake basi Iringa itaendelea kung’ara kitaifa katika usafi. “Tunajua manispaa ya iringa imekuwa na uhaba wa vyombo vidogovidogo vya kuhifadhia taka hasa katika maeneo ya stendi na makutano ya barabara ambapo kuna mkusanyiko wa watu wengi lakini tunaendelea kusisitiza watu wahifadhi taka katika vyom...