Skip to main content

Posts

Showing posts from April 2, 2026

DK TULIA AWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO RUNGWE, ATOA MSAADA WA MCHELE NA FEDHA

Na Mwandishi Wetu Mbeya. Spika wa Bunge Mstaafu, Tulia Ackson, ametoa msaada wa mchele kilo 400 pamoja na Sh4.4 milioni kwa familia 22 zilizoathirika na maafa ya maporomoko ya tope katika Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Dkt Tulia, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Uyole na Rais wa Inter-Parliamentary Union (IPU), alikabidhi msaada huo Aprili 1, 2026 baada ya kutembelea na kukagua maeneo yaliyoathirika kufuatia maporomoko hayo yaliyotokea usiku wa kuamkia Machi 25, 2026, baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali. Katika ziara hiyo, Dkt Tulia alitembelea familia zilizoathirika na kutoa msaada wa chakula pamoja na fedha kwa lengo la kuwafariji wahanga, akisema bado kuna mahitaji makubwa kwa waathirika hao. “Tumetembelea familia katika kata za Lupepo, Kinyara, Ikuti, Kawetele na Nkunga. Hali siyo nzuri—wengi wamepoteza makazi na wanaishi kwa majirani. Wanahitaji chakula, magodoro na makazi bora. Tunawaomba wadau kujitokeza kusaidia,” amesema. Aidha, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Mu...