Skip to main content

Posts

Showing posts from May 26, 2018

DC URGES YOUNG PEOPLE TO DISASSOCIATE FROM BAD MORALS IN THE SOCIETY

Mufindi District Commissioner (DC) Jamhuri William has urged young people who have graduated from basic military training through national service program (JKT) to use their training they received in various camps in the country for national benefit.  Speaking to the graduates during that pass out parade dubbed as ‘Operation Merrerani’ yesterday, DC William urged them to take advantage of the training and knowledge they gained in bringing national development.  He added that youth who were receiving basic military training through national service program to use them to increase employment opportunities through self employment, hence reduce youth unemployment in the country.  “Tanzanian government announced plans to revive compulsory national service to combat moral decay and to teach patriotism…,” said DC William.  Earlier on, service man (SM) Ramadhan Mohamedi who was assisted by service girl (SG) Magdalena Mniko on behalf their graduate...

DC MUFINDI: VIJANA WA JKT MSITUMIE MAFUNZO MLIOPATA VIBAYA

Kikundi cha Singe cha vijana wakijitolea kundi Mererani 2018 wakipita mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakati wa mahafali ya kumaliza mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga taifa (JKT) kikosi cha Maginga JKT wilyani Mufindi, Mkoa wa Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya) MUFINDI: MKUU wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William amsema vijana wanaohitimu mafunzo ya awaliya kijeshi la jeshi la kujenga taifa (JKT) kuyatumia mafunzo wanayoyapata katika kambi mbalimbali hapa nchini kwa faida ya Taifa.  Hatua hii inaelezwa kuwa kama itazingatiwa na vijana wanaohitimu mafunzo ya muda mfupi ya JKT upo uwezekano mkubwa wa taifa kuwa na vijana ambao watakuwa waadilifu pindi watakapokuwa wakilitumikia taifa.  Akizungumza na wahitimu hao jana Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam aliwataka kuyatumia vizuri mafunzo na maarifa waliopata katika kuliletea taifa maendeleo.  Awali, wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi w...

WAZIRI WA MAKAMBA AANDAA MDAHALO NA VIONGOZI WA DINI

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano January Makamba ameandaa mjadala wa Kitaifa kuhusu nafasi ya Dini na uhifadhi wa mazingira utaohusisha Viongozi wa Dini, Wananchi na Viongozi wa Serikali. “Itakuwa ni mjadala wa Kitaifa kuhusu nafasi ya Dini na uhifadhi wa mazingira, tumealika Maaskofu wa dini zote, Waislam pia, sisi tunaamini Watanzania wote tunamuamini Mungu ndo mana tumeona tuwatumie Viongozi wa dini kuelimisha” amesema January Makamba

MPACHIKA MABAO SALAMBA DAU LAKE NI TISHIO

Baada ya kuwabania Yanga kuwapatia mshambuliaji wao hatari kabisa, Adam Salamba, uongozi wa Lipuli FC umetangaza kiasi cha fedha kwa klabu yoyote inayohitaji kumnyakua mchezaji huyo. Taarifa zinaeleza kuwa Lipuli wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 50 pekee ili kumuachia mchezaji huyo aliyekuwa kwenye fomu nzuri msimu huu. Awali Yanga walituma maombi ya kumuhitaji Salamba kwa ajili ya kuwapiga tafu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini yaligonga mwamba kutokana na kanuni za TFF, CAF na FIFA kutoruhusu mchezaji kucheza zaidi ya timu mbili ndani ya msimu mmoja. Inaelezwa kuwa klabu za Simba na Azam FC ndizo zilizoweka nia ya dhati kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo yanaendelea mpaka sasa. Wakati huo Yanga ambao walihitaji nia ya kuwa naye bado hawajazungumza chochote mpaka sasa kama wana lengo la kumsajili au la.

MAWAKILI WA BILIONEA WA ESCROW WACHACHAMAA MAHAKAMANI,WALIA NA UPANDE WA SERIKALI

Didas Respicius, wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Harbinder Seth na mfanyabiashara James Rugemalira, wamekiamsha baaada ya kuwasilisha malalamiko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa washtakiwa hao wamefikisha mwaka mmoja gerezani na upelelezi wa kesi inayowakabili bado haujakamilika. Wakili huyo ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 24, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Iman Mizizi kueleza upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Didas amedai kuwa washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Juni 19, 2017 wakiwa na mashtaka ambayo yanadhaminika lakini wakiwa katika kuwasilisha maombi ya dhamana, walibadilishiwa mashtaka ambayo hayana dhamana. Amesema tangu mwaka jana hadi sasa upande wa mashtaka unadai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kwamba kuwa kwa mujibu wa hati ya mashtaka washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, mwaka 2013.  Ameb...

MINOTI YAENDELEA KUMWAGIKA KWA SHOMARI KAPOMBE

SHOMARI Kapombe ambaye ni beki kisiki wa Timu ya Simba,amemwagiwa fedha na kundi la Spora kupitia WhatsApp linaloshabikia klabu ya Simba ambo ni Mabingwa wa ligi kuu ambayo inafikia tamati. Kapombe amepewa zawadi ya kiasi cha shilingi laki tano (500,000) kama mchezaji bora wa mwezi Aprili 2018. amekabidhiwa kiasi hicho cha fedha na Kiongozi Mkuu wa kundi hilo, Ally Masaninga pamoja na fremu iliyo na picha yake katika Uwanja wa Bocco Vetarani unaotumiwa na wekundu hao wa Msimbazi kujifua kwa ajili ya mechi za ligi. Spora wametoa zawadi ya fedha hizo kama sehemu ya kutoa motisha na hamasa kwa wachezaji wa Simba kujituma zaidi Uwanjani ili kuipigania timu iweze kupata matokeo. Tangu msimu wa 2017/18 uanze, imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kundi hilo kutoa zawadi ya mchezaji bora kwa kila mwezi inayolenga kutia morali kwa wachezaji. Zawadi hiyo imetolewa ikiwa Simba ambao ni mabingwa wapya wa ligi msimu huu wakijiandaa kuhitimisha ratiba ya mechi za...