Skip to main content

Posts

Showing posts from September 14, 2011

DC LUDEWA AITAKA HALMASHAURI KUTUNGA SHERIA NDOGONDOGO ZA MADINI ILI KUJIONGEZEA MAPATO

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa Bi. Georgina Bundala ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kutunga sheria ndogondogo (by laws) ili kujipatia mapato kupitia watafiti na wachimba madini wanaoingia wilayani humo kila kukicha. Bi Georgina aliyasema hayo jana   ofisini kwake alipotembelewa na mwandishi aliyotaka kujua ni nini mchango wa watafiti na wachimba madini waliopo katika maeneo mbalimbali wilayani mwake kwa wilaya yake. Bundala alisema anashangaa kuona Baraza la Madiwani chini ya wabunge wawili wasomi na wanasheria kunyamaza kimya bila kuibua mjadala kuhusu kutunga sheria ndogondogo zitakazoingizia halmashauri yao kipato. “Halmashuri ya Wilaya ya Ludewa inaweza kujiongezea kipato kupitia watafiti na wachimbaji madini waliopo katika maeneo mbalimbali kwa kutunga sheria ndogondogo zitakazo wabana wadau hao,” alisema mkuu huyo. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya L...