Picha/Maktaba Kaimu afisa elimu mkoa wa Iringa, Euzebio Mtavangu amesema kuwa jumla ya watahiniwa 15,818 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari mwaka huu. Mgawanyo wa watahiniwa hao katika halmashauri ni halmashauri ya Manispaa (4,785), halmashauri ya wilaya ya Iringa (3,368), halmashauri ya wilaya ya Kilolo (2,784) na halmashauri ya wilaya ya Mufindi (4,881). Akiongelea matarajio ya ufaulu katika mkoa, Mtavangu alisema kuwa mkoa unatarajia kufanya vizuri na kupindukia matarajio ya BRN ya 80%. Alisema kuwa matarajio hayo yanatokana na mkoa kuwa uliboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Sababu nyingine alizitaja kuwa ni wanafunzi wa masomo ya sayansi kufanya majaribio halisi baada ya kuwa na maabara za kutosha na kufanya ufaulu kwa masomo ya sayansi kuwa mzuri. Aidha, wingi wa walimu wenye shahada umeongeza chachu ya mafanikio katika sekta ya elimu mkoani Iringa. Mkoa wa Iringa umekamilisha maandalizi ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2015...