Binagi Media Group Mapambano dhidi ya ugongwa hatari wa Malaria yameendelea kuonyesha mafanikio mkoani Mwanza, baada ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo kupungua kutoka asilimia 19.01 mwaka 2011/12 hadi asilimia 15.1 mwaka 2015/16. Hiyo ni kutokana na juhudi za serikali kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo shirika la misaada la watu wa Marekani USAID ambalo limeendelea kusaidia vyandarua vyenye kinga kwa ajili ya mapambano dhidi ya malaria. Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi aliyasema hayo jana wakati wa zoezi la kugawa vyandarua bure katika shule ya Msingi Senge iliyopo Kata ya Bujashi wilayani Magu ambalo lilishuhudiwa pia na ujumbe kutoka USAID Marekani. Alisema mbali na kuua vimelea vya Malaria kwa kutumia viuatilifu, pia serikali inagawa vyandarua bure katika shule za msingi, vituo vya afya, zahanati pamoja na hospitali ili kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Monica Ngalula pamoja na Marco Y...