Mafinga. Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Mafinga limepitisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 yenye jumla ya Sh38,651,155,000, katika kikao kilichofanyika Februari 21, 2026, kikilenga kuimarisha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya mji huo. Akiwasilisha rasimu hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Afisa Mipango na Uratibu wa Mji, Peter Ngusa, alisema halmashauri imejipanga kukusanya na kutumia fedha hizo katika utekelezaji wa majukumu ya msingi, miradi ya maendeleo na kuboresha ustawi wa wananchi. Alifafanua kuwa kati ya fedha hizo, Sh8,844,800,000 zinatarajiwa kukusanywa kutoka mapato ya ndani, Sh942,454,000 ni ruzuku ya matumizi mengineyo (OC), Sh23,376,336,000 ni ruzuku ya mishahara, na Sh5,487,565,000 ni ruzuku kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kwa mujibu wa mpango huo, vipaumbele vilivyowekwa ni pamoja na kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, kununua maeneo kwa ajili ya uwekezaji, kuendeleza shamba la parachichi la Makal...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.