Skip to main content

Posts

Majeruhi wa Ajali ya Shabiby na Lori Wasimulia Walivyookoka Kifo Iringa

Baadhi ya majeruhi wa ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Shabiby na lori la mizigo lililokuwa likisafirisha vinywaji baridi aina ya Pepsi wameeleza kwa masikitiko namna walivyookoka katika tukio hilo lililotokea katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Ajali hiyo ilitokea baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso, na kusababisha vifo na majeraha kwa abiria kadhaa. Mwandishi wa The Guardian alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kuzungumza na baadhi ya majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu, huku wengine wengi wakiwa tayari wameruhusiwa baada ya hali zao kuimarika. Mmoja wa majeruhi hao, Juma Shaban, mwalimu wa Songwe Tech Secondary School mkoani Songwe, alisema wakati ajali inatokea alikuwa amelala usingizi ndani ya basi akiwa safarini kuelekea Mbeya. “Nilikuwa nimelala kabisa. Ghafla nikasikia kelele za watu wakivunja vioo vya basi ili kuwaokoa abiria. Nilipojitambua nilikuwa navuja damu nyingi na mguu wangu ulikuwa umevunj...
Recent posts

TFS YASISITIZA MAADILI KAZINI, YATAKA UZINGATIAJI WA MATUMIZI SAHIHI YA MIFUMO

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TFS na Meneja wa Rasilimali Watu, Bahati Mtomaye alisema kuwa matumizi sahihi ya Mifugo pamoja na kuzingatia maadili ni nguzo muhimu katika kuboresha utendaji wa taasisi na kujenga imani kwa umma Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TFS na Meneja wa Rasilimali Watu, Bahati Mtomaye alisema kuwa matumizi sahihi ya Mifugo pamoja na kuzingatia maadili ni nguzo muhimu katika kuboresha utendaji wa taasisi na kujenga imani kwa umma. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya matumizi sahihi ya mifumo katika utendaji. Na Fredy Mgunda, Mufindi WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeanza kuonyesha msimamo mkali katika vita dhidi ya rushwa na ukiukwaji wa maadili kwa kuwataka watumishi wake kuzingatia kikamilifu nidhamu ya kazi na matumizi sahihi ya mifumo ya kiutumishi, hatua inayolenga kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utendaji. Msisitizo huo umetolewa katika siku ya pili ya semina ya mapambano dhidi ya rushwa na maadili kwa maafisa na askari wa Shamba la Miti Sao Hill,...

Land Health Compact Review Meeting in Iringa

  Deputy Country Representative of International Union for Conservation of Nature Tanzania, Anthony Mhagama, makes a presentation on the objectives of the workshop during the Land Health Compact Review Meeting in Iringa. The organisation, in collaboration with partners, is implementing the Sustainability and Inclusion Strategy for Growth Corridors in Africa (SUSTAIN-AFRICA) project.

FESTO KISWAGA ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU KUWANIA UBUNGE ISIMANI

  Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga, amechukua na kurejesha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa Jimbo la Isimani, mkoani Iringa.  Zoezi hilo limefanyika katika ofisi za CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ndani wa chama hicho kuelekea uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.  Kiswaga, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi serikalini, ni miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo ya ubunge, akilenga kurithi kiti kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Isimani, William Lukuvi, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Ajira na Wenye Ulemavu).

Mabalozi Wastaafu Kuongeza Nguvu katika Kuimarisha Demokrasia ya Nchi

Na Mwandishi wetu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeanza kuweka utaratibu wa kutumia hazina ya maarifa na uzoefu kutoka kwa Mabalozi Wastaafu ili kuimarisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kuimarisha diplomasia ya nchi.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo , amebainisha utaratibu huo leo Aprili 15, 2026, jijini Dar es Salaam wakati anafungua kikao cha mashauriano kati ya uongozi wa Wizara na Mabalozi Wastafu.  "Wizara tumeanzisha utaratibu wa kuwa na vikao vya mara kwa mara na Mabalozi Wastaafu ili kuvuna maarifa na uzoefu wao kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ili ulete nanufaa katika nyanja mbalimbali kama vile, siasa, ulinzi na usalama, uchumi, biashara, uwekezaji na utalii". Balozi Kombo alisema. Balozi Kombo ametaja mifano ya maeneo ambayo angependa Mabalozi Wastaafu wachangie maarifa na uzoefu walio kuwa nao ili maeneo hayo yaendelee kuwa na manufaa zaidi kwenye nchi. M...

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI UJENZI WA SOKO LA MACHINGA IRINGA KUANZA

Na Friday Simbaya, Iringa Serikali imeeleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Soko la Machinga Complex katika Manispaa ya Iringa, uliopitishwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maeneo rasmi ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati. Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo, bungeni, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Festo Dugange, alisema mradi huo unatarajiwa kujengwa katika eneo la zamani la stendi ya mabasi, Kata ya Kitanzini, lenye ukubwa wa mita za mraba 6,555 kwa gharama ya Sh bilioni 4.67. Alifafanua kuwa soko hilo litakuwa na vizimba 800, maduka 150 na migahawa 8, na linatarajiwa kuhudumia wafanyabiashara 958, wakiwemo wafanyabiashara wadogo 800, wa kati 150 pamoja na mama na baba lishe 8. Kwa mujibu wa Dugange, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imetenga Sh milioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya ...

POLISI IRINGA WAKAMATA WATUHUMIWA 53, WAONYA TAARIFA ZA UONGO

Na Friday Simbaya, Iringa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limekamata jumla ya watuhumiwa 53 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu katika operesheni zilizofanyika maeneo tofauti kuanzia Aprili Mosi, 2026, huku likitoa onyo kali kwa wananchi dhidi ya utoaji wa taarifa za uongo zinazosababisha taharuki. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, alisema miongoni mwa waliokamatwa ni Ramadhani Mussa (33), dereva mkazi wa Dar es Salaam, aliyetiwa hatiani kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuwa ameibiwa sehemu zake za siri. Kwa mujibu wa Bukumbi, mahakama ilimhukumu Mussa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kuthibitika kuwa taarifa aliyotoa haikuwa ya kweli. “Katika operesheni hizi, tumefanikiwa pia kuwakamata watu wengine waliokuwa wakitoa taarifa za uongo na kusababisha taharuki kwa wananchi,” alisema Bukumbi. Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Mussa Kaundi (39), mfanyabiashara mkazi wa Mafinga, pamoja na wenzake wawili kutoka Isakalilo, M...