Mgombea Daudi Masasi aliyepata kura 21, agoma kusani matokeo kutokana na alichodai kuwa hajaridhishwa na mchako. Mgombea Chiku Abwao aliyepata kura 25, akisani matokeo. ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chiku Abwao ameshinda kura za maoni za chama cha ACT Wazalendo ikiwa ni siku chache toka ajiunge na chama hicho. Ushindi mwembamba wa kura 25 alizopata dhidi ya mgombea mwenzake Daudi Masasi aliyepata kura 21, umemuweka katika nafasi ya kuteuliwa na chama chake hicho kipya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu. Kabla ya kujiunga na ACT Wazalendo, Abwao alipania kugombea ubunge katika jimbo la Isimani kupitia Chadema, lakini kwa kile alichoita hila zilizokuwa zikifanywa dhidi yake na mbunge wa jimbo la Iringa Mjini anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa ndoto yake hiyo imekoma. Kabla ya kushinda kura hizo za maoni Abwao alise...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.