Skip to main content

Posts

Showing posts from April 22, 2011

KONGAMANO LA PASAKA 2011

IGIZO IGIZO VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFURAHIA MAIGIZO Washiriki wa Kongamano la Pasaka 2011 Peramiho ambayo ni wanafunzi wa sekondari na vyuo vya ufundi (TYCS) wakifuatilia maigizo mbalimbali wakati kongamano hilo lililofungiliwa jana na Mhashamu Askofu wa Jimbo Kuu la Songea , Nobert Mtega katika ukumbi wa EMAU. Zaidi ya vijana 300 wanahudhulia kongamano hilo llinaloendelea hivi sasa na litafungwa tarehe 25.04.2011 na Abate wa Abasia ya Peramiho. Akizungumza na mwandishi leo, Mwenyekiti Jimbo na Mlezi wa Tanzania Youth Catholic Students (TYCS), Jimbo la Songea, Abraham Mbunda alisema kuwa waliwaalika vijana karibu mia sita (600), lakini waliofika 300 tu sababu ni mwamko mdogo. Aidha, wanafunzi hao ni kutoka vituo vya LISECO-Lihangano, CHISECO-Chipole, HASECO-Hanga, WISECO-Wimamu, PESECO-Peramiho na SOSECO-Songea.