Skip to main content

Posts

Showing posts from August 15, 2011

HII NDIO HALI HALISI YA USAFIRISHAJI WA NYAMA MJINI LUDEWA

Wakazi wa Mjini Ludewa mkoani Iringa wakisafirisha nyama  kwa kutumia mkokoteni kutoka Machinjio ya Ibani kwenda mabuchani kwa ajili ya walaji kuweza kununua nyama hiyo jana.

VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI LUDEWA WAPATA MAFUNZO JUU YA AFYA YA UZAZI NA MTOTO

Ludewa ZAIDI YA VIONGOZI 53 wa dini mbalimbali wanawake kwa wanaume kutoka katika maeneo mbalimbali wilayani Ludewa, Mkoa Iringa wamehudhuria mafunzo ya siku tatu kuhusu Afya ya uzazi na mtoto. Shirika lisilokuwa la kiserikali la IMA WORLD HEATH la jijini Dar es Salaam limetoa mafunzo hayo maalum kupitia mradi wa Maisha Program uliofadhiliwa na shirika la maendeleo la kimataifa la watu wa marekani USAID. Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mratibu wa mradi huo   Bw Joel Lubebe alieleza kuwa sababu ya kuwapa elimu hii viongozi wa dini mbalimbali ni kutokana na viongozi hao kuaminiwa na jamii, pia jamii kuwa tayari kupokea maagizo na mafundisho yao sanjari na ushawishi na vipawa walivyopewa na Mungu mwenyewe. Bw Lubebe alisema mradi wa Maisha Program unalenga kupunguza vifo vya uzazi vinavyotokana na sababu za moja kwa moja kama kutokwa damu kupita kiasi kwa wajawazito baada ya kujifungua pia kupunguza ...