Skip to main content

Posts

Showing posts from January 11, 2016

LEITCIA NYERERE KUZIKWA BUTIAMA

SUMAYE 'ASHANGAZWA' NA RAIS MAGUFULI KUMJULIA HALI HOSPITALINI

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam jana. Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam jana.

MESSI MCHEZAJI BORA DUNIANI ASHINDA KWA MARA YA TANO TUZO YA BALLON D’OR 2015

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia. Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%. Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo. Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake. Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil. Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita. Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia

PAMBAZUKA NA SIMBAYABLOG NA MAGAZETI YA LEO JUMANNE

KIWIA AONDOA KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA

Agrey Laban ambae ni Katibu wa Highness Kiwia akizungumza na Wanahabari nje ya Mahakama. Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG Mahakama  Kuu Kanda ya Mwanza leo imetupilia mbali kesi ya Kupinga Matokeo ya ubunge  katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea  ubunge katika jimbo hilo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Haighness Kiwia. Katika kesi hiyo ambayo ni namba mbili ya mwaka  2015 iliyofunguliwa Novemba 25 mwaka jana, Kiwia alikuwa akipinga ushindi wa  mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula kupitia Chama cha Mapinduzi CCM  kutokana na madai ambayo ni pamoja na kuendesha kampeni za ubaguzi wa kikabila  sanjari na kupata kura ambazo hazikuendana na idadi ya wapiga kura  walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.  Kesi hiyo imefutwa baada ya Kiwia kupitia kwa  mwanasheria wake Paul Kipeja kuiomba Mahakama kufuta kesi hiyo kwa madai ya  kwamba mtej...

MSIBA DMV NA TANZANIA LETICIA NYERERE HATUKONAE TENA

Leticia Nyerere enzi ya uhai wake Familia ya Leticia Nyerere ya Lanham, MD inasikitika kutangaza kifo cha mama Yao mpenzi kilichotokea tarehe 10 January 2016 nchini marekani. Mipango na utaratibu wa kusafirisha mwili inafanywa. Msiba upo 9004 brightlea court, Lanham MD 20706. Kama mila na desturi zetu tufike kuwafariji familia. Kwa maelezo zaidi wasiliana na : Margareth mageni 240 462 9138 Emmanuel muganda 240 447 2801 Ramadhani kamguna 202 459 3838 Bwana ametoa. Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe

SERIKALI KUTOA BURE MBEGU ZA MTAMA KWA WENYE UPUNGUFU WA CHAKULA

Mkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,  Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amewataka wananchi waliokumbwa na uhaba wa chakula nchini kufuata ushauri wa wataalam kwa kupanda mimea inayostahimili ukame ikiwemo mtama na uwele ili kuondokana na adha hiyo kila mwaka.  Akizungumza jana na wananchi wa vijiji vya Iguluba na Mkulula vilivyopo kata ya Malenga Makali, Tarafa ya Isimani ambayo imeathirika zaidi na upungufu wa chakula wilayani Iringa, Brigedia jenerali Msuya amesema serikali itawapatia wananchi hao mbegu za mtama za bure ili wapande msimu huu. Mkurugenzi wa Idara ya Maafa amefuatana na ujumbe wake kutathmini hali ya upungufu wa chakula wilayani Iringa na kujiridhisha na ugawaji wa msaada uliotolewa na serikali na kujua ni maeneo gani yanahitaji msaada zaidi. Brigedia Jenerali Msuya anawahakikishia wananchi kuwa hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa. Wakielezea hali halisi ya upungufu wa chakula wananchi wameishukuru serikali kwa kupelekea chakula...