Skip to main content

Posts

Showing posts from July 28, 2011

WANANCHI LUDEWA HAWAJUI HATIMA YAO

WAKATI Taifa linadhimisha miaka 50 ya Uhuru wananchi katika Kata za Mundundi na Mkomang’ombe ya Wilaya Ludewa, Mkoa wa Iringa ni zaidi ya miaka miwili sasa wamekaa tu bila kufanya shughuli za maendeleo kutokana na maeneo wanayoishi kuwa ndani ya migodi ya madini ya chuma na makaa ya mawe. Aidha katika hali nyingine maeneo mengi ndani ya Wilaya ya Ludewa yanamilikiwa na watu wasiojulikana kwa kupewa vibali na ofisi ya madini kanda ya mbeya huku wenyeji wakibaki midomo wazi wasijue la kufanya. Hayo yalibainishwa hivi karibuni na madiwani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa walipofanya ziara ya kushtukiza katika Kata ya Iwela na kuwakuta wachimbaji waliodhaniwa kuwa ni wavamizi wakiwa na vibali kamili na ndipo walipofumbuka macho baada ya kuona ramani inayoonesha vibali zaidi ya 70 vilivyotolewa na kamishna wa madini kanda ya mbeya. Ni kutokana na hali hiyo, madiwani katika Baraza kuu walimtaka kamishna wa madini kanda ya Mbeya kufika haraka Ludewa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi ...