Skip to main content

Posts

Showing posts from December 3, 2015

AMKA NA SIMBAYABLOG KWA MAGAZETI YA LEO IJUMAA

MEYA WA MANISPAA YA IRINGA KUZUNGUMZA NA WANAHABARI KESHO

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Iringa, ambaye pia ni diwani kata ya Isakalilo, Alex Kimbe (Chadema) pichani kesho saa 5 asubuhi ataongea na waandishi wa habari ofisini kwake, juu ya mustakabali ya Manispaa ya 2015-2020. Diwani wa kata ya Isakalilo, Alex Kimbe (Chadema) jana alichaguliwa kwa kura 21 kuwa Meya wa Manispaa ya Iringa. Kuchaguliwa kwa Kimbe kumemaliza mvutano wa ndani kwa ndani uliokikumba chama hicho wakati kikiwa katika mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo na kumaliza historia enzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoa Meya kila baada ya Uchaguzi Mkuu. Katika kinyang’anyiro hicho ambacho CCM walikuwa wasindikizaji kwasababu ya kuwa na idadi ndogo ya madiwani; mgombea wake Bashir Mtove alijipatia kura 6. Mtove aliwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na aliyekuwa Meya wa miaka mingi wa manispaa hiyo, Amani Mwamwindi ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, alishinda kwa kura chache kiti cha udiwani wa kata ya Mlandege dhidi ya mgombea wa C...

CHAVITA wamuomba Rais Magufuli awakumbuke

CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Tawi la Mkoa wa Iringa kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakiksha kuwa makundi yote maalumu yanapata haki sawa na mengine ili kuondoa dhana ya ubaguzi. Akiongea na SIMBAYABLOG Katibu wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Shaibu Juma ambapo alisema kuwa wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa kibali cha kufanya sherehe za siku ya Walemavu kitaifa Mkoani Mwanza. Alisema kuwa kuna makundi mengine, yamekuwa yakiwezeshwa mara kwa mara aidha kupitia kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali na hivyo kuweza kupata maendeleo kwa haraka na kumudu maisha yao ya kila siku. Juma alisema kuwa katika Kampeni zake za kutafuta Urais Dkt. Magufuli alisema katika utawala wake hatabagua makundi maalum hasa wenye ulemavu katika uongozi wake hali ambayo imeonyesha dhahiri kuwa amedhamiria kuwasaidia. “Tunampongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kuongoza Taifa la Tanzania na sisi kama makundi ya watu wenye Ulemavu tumeahidi kumpa ushirikiano wa hali ya juu kutokana na u...

Australia Tanzania society donates hospital equipment to Mafinga Hospital

By Friday Simbaya, Mufindi  Mufindi district hospital is now going to reduce the problem of shortage of beds for the pregnant women, after the hospital receiving medical equipment and supplies from Australia Tanzania society (ATS) yesterday.  The overcrowding of pregnant women in the maternity ward with the shortage of beds at the hospital has forced the pregnant women to sleep more than one in one bed and others are left sleeping on the floor.  Speaking to the journalist yesterday the acting medical officer in charge Dr. Abdul Mussa Msuya said that the donation will go a long way in reducing some of the problems the hospital was facing on a daily basis.  He said that lack of hospital equipment and medical supplies was a major barrier for doing surgical operations and limitation of nurses and midwives is also another challenge but with that donations it will help minimize the huge challenge that they face on daily basis.  Dr. ...

RAS: Fufuani mifumo ya kukagua maziwa ili kulinda afya ya mlaji

Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, (RAS) Wamoja Ayubu ametoa wito kwa wakaguzi wa maziwa kutoka mikoa ya iringa, njombe na mbeya kuwa jukumu la ukaguzi wa maziwa ni kazi yao ya msingi na sio kazi ya ziada kwao. Alisema kuwa jukumu la ukaguzi wa maziwa kwa wakaguzi sio kazi ya ziada bali ni kazi yao ya msingi na kusisitiza watoe ushirikiano wa dhati kwa bodi ya maziwa na mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa afrika mashariki (EADD II), ili kujenga na kuimarisa vituo vya mauzo ya maziwa. RAS huyo alitoa rai hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi wa maziwa kutoka mikoa ya iringa, njombe na mbeya yaendelea mkoani Iringa. Alisema kuwa kukagua maziwa ni muhimu sana kwakuendeleza tasnia ya maziwa na kulinda afya ya mlaji na hasa kwa viwanda ili kuweza kusindika maziwa wanahitaji maziwa yaliyo na viwango vya juu vya ubora. “Napenda pia nichukue nafasi hiikuwahamasisha halmashauri zote nchini kuanzisha au kufufua mifumo ya kukagua maziwa ili kulinda afya ya mlaji,” ...

MRATIBU WA UN NCHINI, ALVARO RODRIGUEZ ZIARANI MKOANI SINGIDA KUKAGUA MIRADI YA SHIRIKA HILO

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alipomtembelea na kufanya mazungumzo ofisini kwake jana mjini Singida. Na Modewjiblog team, Singida Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone ofisini kwake kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mkoani humo. Mratibu huyo yupo Mkoani hapa kwa siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Katika siku yake ya kwanza atatembelea mradi wa afya ambao unashughulikia watu wanaoishi na VVU katika kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi. Pia atatembelea kikundi cha ufugaji nyuki kinachojihusisha na uzalishaji wa asali na utengenezaji wa mishumaa. Aidha akiwa kijiji cha Puma atatembelea kambi waliokolazwa watu wenye ugonjwa wa Kipin...

MELI MPYA YA MV MAPINDUZI YAWASILI KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR, IMETOKA KOREA

Meli Mpya ya MV Mapinduzi Ikiwasili katika Bandari ya Zanzibar Ikitokea Nchini Korea Ilikotengenezwa. Meli Mpya ya MV Mapinduzi 2 ikiwasili Zanzibar ikitokea Nchini Korea Meli Mpya ya MV Mapinduzi ikiwasili katika bandari ya Zanzibar ikitokea Nchini Korea baada ya kukamilika kwa Uundaji wake uliochukua miezi 18, ikiwa katika bahari ya Zanzibar ikielekea katika bandari kwa ajili ya ufungaji wa gati katika bandari ya Malindi Zanzibar. Wananchi wa Zanzibar wakiipokea Meli yao Mpya ya MV Mapinduzo 2 wakiwa katika bustani ya Forodhani Zanzibar. Wananchi wa Zanzibar wakichukua picha kupitia simu zao Meli Mpya ya MV Mapinduzi wakati ikiwasili Zanzibar katika bandari ya Zanzibar Meli Mpya ya Mv Mapinduzi 2 ikiwa katika bahari ya Zanzibar. Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika bustani ya forodhani wakiipokea Meli yao Mpya ya MV Mapinduzi 2 ikiwasili Zanzibar ikitokea Nchini Korea ilioundwa meli hiyo. Wananchi wa Zanzibar wakichukua picha kupitia simu zao Meli Mpya ya MV Mapinduzi wa...