SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA (SHIVYAWATA), ambalo ni muungano wa vyama tisa vikuu vya kitaifa vya watu wenye ulemavu tofauti nchini vinampongeza Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Serikali ya Baraza La Mapinduzi Zanzibar 2010 – 2015. Halikadhalika muungano huo wa vyama vinampongeza Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na chama chake Chama cha Wananchi (CUF) kwa kuchaguliwa kuwa mshindi wa pili kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), lakini pia kwa busara aliyoionyesha ya ukomavu wa kisiasa kwa kukubali matokeo na kuepusha vurugu ambazo zingeweza kutokea kama angeamua vinginevyo. Kukubali kwake matokeo si kwamba kumeepusha vurugu tu, bali pia kumeepusha maafa na ongezeko kubwa la watu wenye ulemavu, lakini pia ifahamike kuwa machafuko yoyote yatokeapo waathirika na wahanga wakuu wanakuwa ni watu wenye ulemavu, akinamama, wazee na watoto, hivyo basi Mwenyekiti –SHIVYAWATA Lupi Maswanya Mwaisak...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.