Skip to main content

Posts

Showing posts from September 20, 2011

MADEREVA WAASWA KUZINGATIA ALAMA ZA BARABARANI

Na Vicky Macha, Iringa. MADEREVA wanatakiwa kuzingatia alama za barabarani ili kukabiliana na ajali za mara kwa mara  hasa zinazojitokeza katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TANZAM). Rai hiyo ilitolewa jana na Mkandarasi wa Mradi wa ujenzi wa barabara kutoka makao makuu (Tanroads) Kenfas Mahenge wakati wa makabidhiano rasmi ya barabara hiyo na  makandarasi wa kampuni ya Aarsleff- Interbeton Denmark mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara hiyo mwishoni mwa wiki. Mahenge alisema hali ya nchi ilivyo ambayo ni ya milima, miteremko na kona nyingi hasa katika maeneo ya hifadhi ya wanyamaMikumi ni lazima kila dereva kuzingatia alama hizo pindi apitapo katika barabara hiyo kwani kumekuwa na ongezeko la ajali zinazoendelea kuwatafuna wananchi hasa abiria. Alisema kwa kuliona hilo walilazimika kumtaka mkadarasi kuweka kila eneo alama ikiwemo matuta, lakini kumeoneka  madereva kuendesha magari kwa uzoefu mba...

"Tanga Fresh Ltd" yakumbwa na changamoto mbalimbai katika uzalishaji maziwa

Na Gustav Chahe, Tanga Kiwanda cha uzalishashi maziwa “ Tanga Fresh Limited ” kilichopo Mkoani Tanga kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa zao la maziwa hali inayotokana na ukosefu wa malisho kwa ng’ombe hasa kipindi hiki cha kianzazi. Akiongea na mwandishi wa habari hizi kiwandani hapo hivi karibuni, afisa habari wa kiwanda hicho Bw. Charles Tumaini ameeleza kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinalazimika kujiendesha kwa hasara kutokana na kushindwa kufikia asilimia 100 ya uzalishaji kulingana na nguvu ya mitambo iliyopo. “Kwa sasa uzalishaji ni asilimia 60 tu ambayo sawa na lita 50,000 tu kwa masaa 8, hatujafikia kiwango cha asilimia 100 ya uzalishaji kulingana na nguvu ya mitambo yetu; kwa sasa tunazalisha asilimia 60 tu ambayo sawa na lita 50,000 kwa muda wa masaa 8 kila siku” alisema Bw. Tumaini. “Tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatukwamisha kuzalisha maziwa kwa wingi ambazo miongoni mwake ni kukosa malisho, maji ...