Skip to main content

Posts

Showing posts from December 20, 2015

HOSPITALI ZAAGIZWA KUTENGENEZA MFUMO WA MALIPO WA KIELEKTRONIKI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahi jambo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga (kulia) wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mwishoni mwa juma mkoa wa Lindi.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog ) Na Mwandishi wetu, Mtwara NAIBU Waziri katika Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza kubadilishwa kwa mifumo ya utawala, malipo na uendeshaji katika katika hospitali nchini ili kuleta ufanisi na tija. Akizungumza katika ziara yake ya kujifunza kuona katika hali ya kawaida huwa zinatolewaje katika hospitali za wilaya na mikoa alisema kukosekana kwa mifumo bora ya malipo na motisha kumedumaza utumishi. Ziara yake hiyo ambayo aliifanya katika hospitali ya mkoa wa Lindi ya Sokoine na Ile ya Mtwara ya Ligula ililenga kuona masuala mbalimbali yanayohusiana na utoaji huduma ili kuwa na nafasi ya kutengeneza...

MAHAKAMA YAFUTA KESI YA KUPINGA UBUNGE WA KUBENEA

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imefuta kesi ya madai ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubungo. Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Masaburi dhidi ya mbunge wa jimbo hilo, Saed Kubenea (CHADEMA). Uamuzi wa maombi ya kufuta kesi hiyo uliwasilishwa mahakamani hapo juzi na wakili wa Dk. Masaburi, Clement Kihoko mbele ya Jaji Lugano Mwandambo. Wakili Kihoko alisema kuwa mteja wake hana nia ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo ya kupinga matokeo. Baada ya kuwasilisha maombi hayo, Jaji Mwandambo alisema mahakama imepokea maombi hayo ya kuifuta kesi hiyo. GHARAMA Baada ya jaji kukubali ombi hilo, Wakili Kihoko aliiomba mahakama kuwapunguzia gharama za uendeshwaji wa kesi ya msingi pamoja na fidia ya usumbufu. Hata hivyo, Wakili wa Kubenea, Nyaronyo Kicheere, alisema licha ya upande wa utetezi kuomba punguzo hilo, lakini wanapaswa kulipa gharama hizo. Kutokana na hali hiy...

MAGAZETINI LEO JUMATATU

WAZIRI UMMY MWALIMU AVAMIA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO MKOANI TANGA, KUKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya (jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi) wa dirisha la dawa katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza mchana wa leo Disemba 20, 2015. -Atoa wiki mbili wawe wamefunga mashine ya kukusanya mapato kwa njia ya Kielektroniki ili kudhitibiti upotevu wa mapato yanayotokana na wananchi kuchangia huduma za afya. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wakina mama anayemhudumia mwanae katika wodi ya watoto Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza leo mchana Disemba 20, 2015. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa akina mama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi wakati wa ziara ya kushtikiza aliyoifanya mchana wa leo Desemba 20, 2015 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mk...