Skip to main content

Posts

Showing posts from December 24, 2012

SEASONAL GREETINGS

PEAWA SACCOS YAPATA HASARA YA SHILINGI MILIONI MOJA

Na Friday Simbaya, Songea Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Peramiho (PEAWA SACCOS) kimepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni moja kwa mwaka unaoishia 31/12/2011 kutokana na sababu mbalimbali pamoja na baadhi ya wanachama kutorejesha mikopo kwa wakati. Hayo yalibanishwa na meneja wa PEAWA SACCOS Nestory Mbena Jumamosi wakati akisoma taarifa ya ukaguzi kama ulivyokaguliwa na COASCO Songea kwenye Mkutano Mkuu wa Sita wa mwaka ulifanyika Peramiho katika Wilaya Songea, mkoani Ruvuma. Alisema kuwa hasara hiyo pamoja na mambo mengine imetokana na wanachama waliokopa mikopo kuchelewesha kurejesha kwa wakati na wengine kutorejesha kabisa. Meneja huyo aliongeza kuwa jumla yawadaiwa sugu 14 walipelekwa kwenye kampuni ya kukusanya madeni ya Yono ya Songea na baadhi ya wadaiwa wameanza kulipa baada ya kupelekwa mahakamani. Alisema kuwa jumla ya mikopo iliyotolewa kwa wanachama katika kipindi cha kuishia Novemba 2012 ni 34 yenye thamani ya Tsh. 41,362,340/-. “Jumla ya wa...