Na Friday Simbaya, Iringa MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amewaasa wanafunzi wa kidato cha nne kuzingatia elimu na kusoma kwa bidii, kwa kuwa elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao. Rai hiyo aliitoa alipokuwa akitoa nasaha katika mahafali ya kidini kwa wanafunzi zaidi ya 50 wa umoja wa wakikristo wa wanafunzi Tanzania (UKWATA) yaliyofanyika jana katika Kanisa la KKKT Usharika wa Nyamhanga mjini Iringa. Ibada maalum ya kuwaombea wanafunzi hao kutoka shule za sekondari za Efatha, Ipogolo, Tagamenda na Cagrielo katika Manispaa ya Iringa iliongozwa na Mchungaji Nuru Makweta kwa kushirikiana na Mchungaji Yekonia Koko ambaye pia mlezi wa UKWATA mkoa wa Iringa. Mgeni rasmi Jesca Msambatavangu aliwataka wanafunzi hao wanapopata fursa ya kusoma waoneshe bidii darasani ili wajikomboe ili kutimiza malengo yao ya baadaye. “Lazima muwe na maono ya mbali yakutaka kuwa kina nani hapo baadaye katika taifa hili,”alisisitiza...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.