Skip to main content

Posts

Showing posts from March 26, 2015

JEMBE FM YA MWANZA YAPEWA LESENI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni kwa redio ya Jembe FM ya jijini Mwanza kwenye ofisi za makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog ). Na Mwandishi wetu MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma ametaka matumizi sahihi ya masafa ya radio yanayatumiwa kurusha vipindi vya radio kwa ajili ya maendeleo ya umma.

TAHARIRI: TABIA HII YA WAUZA MITUMBA SOKO LA MCHIKICHINI NI UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam. Na Andrew Chale wa Modewji blog Miongoni mwa mambo ya aibu katika jamii ni pamoja na masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ukiwemo ule wa maungoni hasa kwa wanawake. Kwa muda mrefu mtandao huu umekuwa ukifuatilia vitendo hivyo vibaya kwa jamii vinavyofanywa na watu waliokosa ustaarabu hasa jamii ya vijana katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi karibu maeneo mengi ikiwemo jiji la Dar es Salaam.  Miongoni mwa eneo linaloongoza kwa kuwadhalilisha wanawake ni eneo la soko la Mchikichini lililopo Ilala Mkoa wa Dar es Salaam. Mtandao huu umekuwa ukishuhudia vitendo hivyo vibaya kwa jamii ambapo wengi wa vijana wamekuwa wakifanya kwa makusudi kuwadhalilisha wanawake hasa wasichana wadogo kwa kuwashika maungoni (makalio, kifua/maziwa) huku wakiwalazimisha kununua bidhaa zao. Vitendo hivi vimekuwa ni kama mchezo wa kawaida kwani vijana hao wamekuwa wakiendeleza hali...