Skip to main content

Posts

Showing posts from August 26, 2011

WALIMU WA VYUO VYA UFUNDI STADI WAPIGWA MSASA KUHUSIANA NA CBET

Walimu zaidi ya 30 wa vyuo mbalimbali vya ufundi kutoka katika mikoa ya nyanda za juu (Iringa na Ruvuma) wamefanya semina ya mafunzo yaliyodumu kwa takribani wiki mbili kwa lengo la kujengewa uwezo wa namna ya kutumia mfumo mpya wa kufundishia ujulikanao kama ‘Competence Based Education and Training’ (CBET). Akizungumza na gazeti la Mwenge, Mratibu wa vyuo vya ufundi stadi vya VETA wa nyanda za juu Bw. John Mwanja amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha walimu wa vyuo vya ufundi stadi kutumia mfumo mpya wa kufundishia yani CBET. Mfumo huo mpya wa kufundishia (Competence Based Education and Training (CBET) unatafsiriwa kuwa ni umiliki na uendelezaji wa ustadi, ufahamu, mitazamo sahihi pamoja na uzoefu ili kujiletea mafanikio katika utendaji wa majukumu ya kimaisha. Bw. Mwanja amesema, endapo mfumo huu mpya utatekelezwa kama ilivyokusudiwa, basi utaleta mafanikio chanya zaidi ukilinganishwa na ule mfumo uliokuwa ukitumika hapo awali kutokana na ukweli kwamba mfumo huu mp...