Thomas Joseph Odhiambo Mboya (pichani), alikuwa ni mmoja wa waasisi wa Chama cha Kenya African National Union (Kanu) Wakati anauawa, Tom Mboya, alikuwa ni Waziri wa Mipango ya Uchumi na Maendeleo. Pia alikuwa ni mwanasiasa aliyepewa nafasi kubwa ya kuja kuwa rais wa nchi hiyo baada ya Kenyatta. Mboya alizaliwa Agosti 15, 1930 huko Kilima Mbogo karibu na Mji wa Thika katika maeneo ambayo wakati ule yalikuwa yanaitwa White Highlands. Alisoma na kupata elimu ya juu, akaenda Uingereza na kurejea Kenya mwaka 1956 akafanya kazi na kujiunga na siasa. Wakati huo Waingereza walikuwa wanajaribu kulidhibiti wimbi la wapigania uhuru wa Mau Mau, waliokuwa wanataka ardhi yao na uhuru wa Kenya. Aliajiriwa na Halmashauri ya Jiji la Nairobi, akajiunga na Chama cha Wafanyakazi cha African Staff Association na kuchaguliwa kuwa rais wa chama hicho ambacho kikaitwa Kenya Local Government Workers Union. Aliingia katika bunge ambalo miongoni mwa wabunge 50, Waafrika waliku...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.