Skip to main content

Posts

Showing posts from October 25, 2011

ASKOFU MTEGA

Na Basil Makungu, Ludewa   IKIWA imetimia zaidi ya wiki moja tangu kuuawa kwa Rais wa zamani wa Libya Muamar Gadaffi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Norbert Mtega amewataka viongozi wa Afrika kujali na kuheshimu haki za raia wao kwani mwenye kuua kwa upanga hufa kwa upanga. Askofu Mkuu Mtega aliyasema hayo jana katika Misa ya shukrani na sherehe yake ya kutimiza miaka 25 ya uaskofu iliyofanyika katika Parokia ya Yesu Kristo Mkombozi, lililoko mjini Ludewa mkoani Iringa. Askofu Mtega alisema yeye anachukia sana viongozi wenye dhuruma kwa raia wake na kuwataka viongozi wa Afrika kuacha ubabe, kuacha unafiki na kwamba tukio la Libya liwe changamoto kwao na kuwataka waache kuendesha nchi kama asasi binafsi kwani wananchi wanapochoka kwao kila kitu ni silaha. “Tazameni na oneni enyi viongozi wa Afrika jinsi kiongozi mwafrika ambaye amepewa nafasi na dhamana ya kuongoza wananchi anavyoweza kukosea na kupitiwa kwa ulevi wa madaraka huku anasema yeye anawapenda watu...